Breaking News



Mjue Felix Erasto Mshomi ni nani katika kuwezesha maendeleo ya Jamii Mkoani Singida.


Na Sylvester Richard.

Felix Erasto Mshomi ni  mfanyakazi wa ShirikaShirika la (AEE) African Evanjilist Enterprises  lenya makao yake makuu Dar es salaam Nchini Tanzan . Anaeleza kuwa shirika hilo limeanza kutoa msaada katika maendeleo ya jamii kwa kutoa mafunzo ya ujasiliamali hapa Mkoani  Singida  tangu mwaaka 2007 kwa kupitia wawezeshaji wa  vikoba ambapo Shirika hilo limekuwa likifadhiliwa na (NCA) Norwegian  Church Aid.

Akiongea na Machibya blog, Felix ameeleza kuwa ni miaka 8 sasa tangu Shirika hilo lianze kufadhili mafunzo ya ujasiliamali kwa wawezeshaji wa vikoba Mkoani Singida, kwa kuwezesha mafunzo hayo,  limetia hamasa kubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Singida na mpaka sasa kuna vikundi vya VICOBA 180 vikiwa na wanachama zaidi ya 3000  ambavyo vimekuwa vikipata mafunzo  chini ya ufadhili wa AEE Shirika ambalo huwafadhili kwa mafunzo tu na wanavikoba hujitengenezea mtaji wao wenyewe na husimamia na kukopeshana wenyewe kwa riba ndogo ambapo ndiyo faida ya mafunzo hayo.

Mwaka 2016 kuanzia 06 Juni hadi tarehe 09 Juni AEE  imeendesha mafunzo kwa wajasiliamali 108 waliotoka katika vikundi mbalimbali vya VICOBA vilivyopo Singida.

 Mwaka 2015 Octoba Shirika AEE lilipata mradi uliofadhliwa na UN ambao unawalenga akinamama na unajulikana kama UN WOMEN ECONOMIC EMPOWERMENT PROJECT kwa ajili ya akinamama na mabinti wa Singida ambapo mafunzo yanayofanyika ni mwendelezo wa huo mradi ambao una sehemu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo akinamama na pia una sehemu ya ujenzi wa jengo ambalo litatumika katika kuongeza thamani ya bidhaa kwa mfano kutoka karanga kuwa peanut butter, au kutoka nafaka kama vile mahindi, mtama na uwele kuwa ungalishe kwa ajili ya lishe, kusindika asali, kuichuja na kuipaki ili kuweza kuiuza na hivyo kuwa chanzo cha vipato vyao. Jengo hilo linajengwa katika maeneo ya  Iitit ambapo wanavicoba wa Singida wameweza kuchanga na kununua kiwanja hicho na kupitia ufadhili wa UN sasa jengo liko katika hali ya kumalizia. Aliyataja kuwa ni mafanikio makubwa.


Alieleza kuwa mafunzo yaliyoendeshwa  ni mafunzo ya ujasiliamali na  stadi za biashara kwa ajili ya wakulima na wafanyabiashara na vikundi vya wasindikaji ambao wapo kwenye vikundi vya vikoba hapa Singida ambavyo vinajulikana kama (IR) INTER RELIGION   vikoba ikimaanisha kwamba vikundi vyo vikoba hivyo havifungani na dini yeyote kwahiyo kila mtu anaruhusiwa kujiunga navyo .

Alieza changamoto walizozipata kama wawezishaji ni wahudhuliaji ni wengi kuliko uwezo kwani walikuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa makina mama 100 lakini iliwalazimu kutoa mafunzo kwa watu 108 na kuongeza kuwa kozi ni nzuri wawezeshaji wanaotoa mafunzo haya ni watu kutoka  SUA katika kitengo cha muungano wa walimu wakufunzi wa SUA kinaitwa SUGEKO na walimu kutoka Sido Singida ambao ni watalaamu na wametoa mafunzo mazuri na kwa wakati  na wanasemina wamefurahia saana mafunzo hayo na ndiyo mafanikio.  

Alitanabaisha kuwa awamu ijayo wataboresha kwa kutegemea ufadhili kwani vikoba ni njia ya kumwokoa na kumuinua mjasiliamali mdogomdogo kwa maana hujijengea mtaji wake mwenyewe halafu hujipatia mtaji na kukopeshana wenyewe kwa wenyewe kwa riba ndogo bila usumbufu.

Kisha alitoa wito kwa wale ambao bado hawajajiunga basi wajiunge na vikoba si kwa akinamama tu bali hata akinababa wajitokeze ili wajinufaishe na vikundi hivyo.

Naye Mratibu wa VICOBA Mkoani Singida Ndugu Happy Fransis alieleza kuwa ni mafanikio makubwa wameyapata kupitia VICOBA tangu vikundi hivyo vianzishwe yakiwa ni pamoja na kupunguza wimbi la mabinti kwenda kutafuta kazi za ndani, Akinamama wameachana na maisha tegemezi kwa waume zao kwa kila kitu, Kupata ada za Shule za Watoto wao na baadhi wamejenga nyumba bora. Aliwataka wananchi wa Singida bila kubagua jinsia wajiunge na VICOBA visajiliwe ili waendelee kunufaika kwa pamoja.




Toa maoni yako kwa kupitia anwani zifuayazo
Email;        sylvestermac87@gmail.com
                  Machibya.richard@yahoo.com
Facebook  - Machibya Richard
Sim ;          0768 367 454
                    0652 683 063

No comments