SHIRIKA LA AEE LAWEZESHA VIKOBA
180 SINGIDA.
Na. Sylvester Richard.
Shirika
la (AEE) African Evanjilist Enterprises
lenya makao yake makuu Dar es salaam Nchini Tanzani limeendesha mafunzo
ya ujasiliamali kwa wanavicoba 108 waliowakilisha vikundi vyao vilivyopo Mkoani
humo chini ya ufadhili wa Shirika
lisilokuwa la kiserikali la (NCA)
Norwegian Church Aid lenye Makao yake
Makuu Nchini Norwey mafunzo ambayo yaligawanyika katika makundi matatu ambayo
ni wafanyabiashara, wakulima na wasindikaji wa bidhaa.
Aidha
mafunzo hayo yalifanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mkoani Singida
na yalifunguliwa tarehe 06.06.2016 na
kufungwa rasmi tarehe 09.06.2016 majira ya saa 11:00 jioni ambapo Mgeni rasmi
akiwa ni Mh. Hana Churi Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Singida.
Katika
hotuba yake Mgeni rasmi aliwaasa wanasemina kuwa wanatakiwa kwenda kuyafanyia
kazi mambo waliyojifunza kwa muda wote walikuwepo Chuoni hapo ikiwa ni pamoja
na kwenda kuvishirikisha vikundi walivyoviwakilisha.
Mgeni
Rasmi alieleza kuwa Serikali ina mikakati ya kuwezesha vikundi vya vikoba kwa kuvipatia
mikopo yenye riba nafuu ambapo aliwahamasisha wananchi kujiunga na vikundi hivi kwani ni rahisi kuvisimamia kwakuwa hujisimamia wenyewe kwa kukutana kila wiki hali ambayo husaidia kuwa na
mawasiliano ya karibu kwa wananvikoba ambapo hata mikopo inapotolewa huweza
kurejeshwa haraka na kuweza kukopesha tena kwenye vikundi vingine tofauti na
vikundi vingine vinavyosikia tu kwamba Halimashauri inatoa mikopo vinaundwa si
rahisi kuvisimamia kwani vinasambaratika kwa urahisi kwa maana havina usimamizi
madhubuti.
Kuhusiana
na masoko ya bidhaa zinazizalishwa na vikundi, Mgeni Rasmi aliwaasa wanasemina
kwenda kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ili ziweze kuingia kwenye
soko zenyewe kwa kupitia mafunzo waliyoyapata. Pia aliwataka wapeleke bidhaa
zao katika maonyesho mbalimbali kama vile Maonyesho ya NANENANE na SABASABA ili
kuweza kutangaza bidhaa zao na kuwaze kununulika kwa haraka. Hata hivyo alisema
yeye yuko tayari kwenda kushauriana na uongozi ili kuona jinsi ya kupata masoko
ya uhakika.
No comments