Ajali ya Gari yatokea Mlima Sekenke Mkoani Singida na kusababisha kifo cha Dereva na majeruhi. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Simoni S. Haule awaasa madereva wote kuendesha magari yao kwa kufuata Sheria,kanuni na taratibu za usalama barabarani.
JESHI LA POLISI TANZANIA
OFISI YA KAMANDA WA POLISI
“M” SINGIDA
07.06.2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
(PRESS RELEASE)
AJALI YA GARI KUACHA NJIA , KUPINDUKA NA KUSABABISHA
KIFO NA MAJERUHI.
Mnamo terehe 06.06.2016 majira ya saa 11:00 alfajiri
huko katika maeneo ya Mlima Sekenke, Kata ya Ulemo, Tarafa ya Kinampanda ,
Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida barabara kuu ya Singida – Nzega, Gari lenye
namba T.724 BHU/T.733BRJ SCANIA TREILER
mali ya Erick s/o Johanseni ,
mkazi wa Mulebe Mkoani Kagera, likiendeshwa
na Dereva aitwaye David s/o Sailes @
Kibuga, Mhehe, (31, mkazi wa Dar es salaam akiwa amepakia mzigo wa cement
akitokea Dar es salaam kwenda Mureba aliacha njia kupinduka na kusababisha kifo
cha Mtu mmoja na majeruhi kwa watu
wawili.
Aidha aliyefariki katika ajali hiyo ni Jackson s/o
Sailes @ Kibuga ambaye ni abiria katika gari hilo ambapo waliojeruhiwa ni David s/o Sailes @ Kibuga, Mhehe, (31), mkazi
wa Tegeta Dar es salaam ambaye amepata
majeraha sehemu za kifua na kiunoni na Medhod s/o
Nyamba, (26), Tingo ambaye amepata majereaha usoni na miguuni,
Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Iramba hali kadhalika Mwili wa marehemu
umehifadhiwa hospitalini hapo ukisubiri
taratibu za mazishi. Chanzo cha ajali hiyo kimebainika kuwa ni kufeli kwa breki
za gari hilo.
AJALI YA GARI KUGONGA GARI
JINGINE NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU.
Tarehe 06.06.2016 majira ya saa 13.15 huko Maeneo ya Namfua, katika Barabara ya Siangida
Dodoma, Gari yenye namba SM 9110 TOYOTA LAND CRUISRE mali ya Manispaa ya
Singida ikiendeshwa na Dereva aitwaye Salim s/o Ramadhani, (54), Mnyauru mkazi
wa Kindai, Tarafa ya Mungumaji, Wilaya na Mkoa wa Singida, akitokea katika Kituto
cha Afya Sokoine kilichopo Manispaa ya Singida akiwa amebeba mgojwa aliacha njia na kuligonga
gari jingine lenye namba T.341 BCH CARINA ilkiendeshwa na Hamisi s/o Iddi,
(66), Mnyamwezi mkazi wa Majengo Singida.
Aidha katika ajali hiyo watu wanne walipata majeraha.
Majeruhi hao ni pamoja na Salim s/o
Ramadhani dereva wa gari namba SM 9110 TOYOTA LAND CRUISER, Bertha d/o Athanas,
(23), Mnyaturu, Mkazi wa Kindai ambaye ni mgonjwa akitokea katika Kituo cha
Afya Sokoine kuelekea Hospitali ya Rufaa
Singida, Rehema d/o William, (27) msaidizi wa mgonjwa na Mary s/o Temalilo, (50), ambaye ni Muuguzi wa Kituo cha Afya Sokoine.
Majeruhi wote wamepatiwa matibabu katika Hospitali ya
Rufaa Singida, hali zao zinaendelea vizuri ambapo Majeruhi watatu wameruhusiwa
isipokuwa Bertha d/o Athanas bado anaendelea kupata matibabu Hospitalini hapo
na hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi la Polisi limefanya uchunguzi wa awali wa ajali
hiyo na kubaini chanzo chake kuwa ni uzembe wa Dereva Salim s/o Ramadhani ambaye alihama katika
upande wake na kilifuata gari jingine na hivyo kasababisha ajali hiyo ambapo
anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa madereva wote wa
vyombo vya usafiri kuendesha vyombo vyao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu
za usalama barabarani. Madereva pia wanatakiwa kukagua magari yao
kabla ya kuanza safari ili kubaini ubovu wa magari yao na kurekabisha kabla ya kuanza safari ili
kuepusha ajali zisizokuwa za lazima.
Imetolewa na ;
SIMON S. HAULE – ACP
Kny; KAMANDA WA POLISI (M)
SINGIDA
No comments