MKOA WA MWANZA WAONGOZA MASHINDANO
YA MBIO ZA BAISKELI ZILIZOFZNYIKA TAREHE 21.05 2016 MKOANI SINGIDA
Mkoa wa mwanza waongoza katika
mashindano ya mbio za baiskeli yaliyoandaliwa na Chuo cha Uhasibu Tanzania
(TIA) Tawi la Singida kwa kushirikiana na Friebds & Family connection yenye Makao
yake makuu San Diego Nchini Marekani na kudhaminiwa na Banki ya NMB, KAMPUNI YA
BIA YA SERENGETI, GEARING FOR HOPE NA FUTURE HERITAGE kwa lengo la kuhamasisha
uchangiaji wa fedha kwa ajiri ya watoto wanaoishi katika madhingira magumu
wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi
(ALBINO).
Mgeni rasmi katika mashindano
hayo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mh. Saidi Amanzi ambaye aliwashukuru
waandaaji wa mashindano hayo kwa kuandaa mashindano yaliyolenga kuhamasisha uchangiaji wa fedha ili kuwawezesha wahitaji wa vituo vitatu
ambavyo ni Kituo cha Urambo Tabora chenye watoto 80, Singida Day Center chenye
watoto 800 na Ujejenzi wa vyumba katika Chuo cha Uhasibu (TIA) Tawi la Singida.
Mgeni rasmi aliwashukuru pia washiriki wa mashindao walioshiriki mwaka huu na kutoa wito kwa
wananchi kujitoa kwa wingi katika mashindano kama hayo yatakayofanyika tena mwaka
2017 Mkoani Singida na pia aliwaomba wananchi kujitoa kwa hali na mali
ili kuchangia watoto husika ili waweze
kupata mahitaji yao ya msingi na kuishi vizuri.
Aidha mashindano yaligawanyika
katika makundi manne ambayo ni 1, Kundi la watoto ambao wailikimbia umbali wa
Km 10, Kundi la wananwake ambao walikimbia umabali wa Km 18 na Kundi la wanaume
ambao walikimbia umbali wa Km 24, na 4 ni kundi la wanafunzi ambapo washindi wa
kwanza walijipatia kitita cha Tsh. 500,000/= na washindi wa pili alipata Tsh.
300,000/= na washindi watatu walipa tsh. 100,000/=
Nafasi ya kwanza kwa Watoto
ilichukuliwa na watu wawili kutokana na
sababu za kiufundi zilizojitokeza. Washindi haoni Amour Husen na Abeid Selemani
wote Kutoka Mkoani singida hali kadhalika mshindi wa watatu alitoka katika
Mkoa huo. Kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Laurencia
Luzuba Kutoka Mkoa wa Mwanza na
nafasi ya pili mshiriki kutoka Mkoa wa
Arusha na watatu alitoka Mkoa wa Singida. Mshindi wa kwanza kwa Kundi la
wanaume ni Masunga Duba kutoka Mkoa wa Mwanza ambapo mshindi wa pili alitoka
Mkoa wa Shinyanga na Mshindi wa kutoka Mkoa wa Singida.
Na .
Sylvester
Richard .
No comments