Somahapa kuhusu Watu wawili wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Singida kwa makosa ya Kubaka na Muaji. Tamaa za kimwili na ulevi wa pombe vikiwa ndiyo vyanzo vya matukio hayo.
THOBIAS G. SEDOYEKA –
ACP
JESHI LA POLISI TANZANIA
OFISI
YA KAMANDA WA POLISI “M” SINGIDA
30.05.2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
(PRESS
RELEASE)
KUBAKA
Tarehe 29.05.2016 majira
ya saa 6:30 mchana Huko katia Kijiji na Kata ya
Iguguno, Tarafa ya Kinyangiri, Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida Mtoto
wa kike mwenye umri wa miaka 11, jina lake linahifadhiwa ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la tano katika Shule ya Msingi Mwando alibakwa na Kulwa s/o Dotto
@Bihume, Mnyamwezi, (21) Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Simbalungwala
katika Wilaya ya Iramba na kusababishiwa
maumivu makali sehemu zake za siri.
Uchunguzi wa awali wa
Polisi umebaini mbinu aliyoitumia mtuhumiwa ni kumvizia muathirika akiwa
anatoka dukani na kisha kumvutia vichakani mahali ambapo alifanikisha ubakaji
huo.
Chanzo cha tukio hilo kimebaininika kuwa
ni tamaa za kimwili za mtuhumiwa ambapo mtuhumiwa huyo amekamatwa na
anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi na baada ya uchunguzi kukamilika
atafikishwa Mahakamani ambapo Muathirika alipatiwa matibabu katika Hospitali ya
Mkoa Singida, ameruhusiwa na hali yake inaendelea vizuri.
MAUAJI
Mnamo tarehe 28.05.2016
majira ya saa 1:30 usiku kaika Kijiji na Kata ya Mkiwa, Tarafa na Wilaya ya
Ikungi, Mkoa wa Singida Joseph s/o Simon, (39), Mnyaturu, Mkulima na mkazi wa
Mkiwa aliuawa kwa kuchomwa na Kitu chenye ncha kali mdomoni karibu na kidevu na
Rajabu s/o Omary, (46), Mnyaturu Mkulima na Mkazi wa Mkiwa wakati wakinywa
pombe za kienyeji nyumbani kwa Mtuhumiwa.
Chanzo cha tukio hilo kimebainika kuwa ni
ugomvi uliotokea baina ya Marehemu na Mtuhumiwa
kutokana na ulevi wa pombe za kienyeji. Imebainika kuwa Mtuhumwa na
Marehemu hawana mahusiano yoyote bali walikutana tu hapo kwenye pombe na ndipo
tukio hilo
lilipotendeka.
Aidha kuhusiana na tukio
hilo mtuhumiwa Rajabu s/o Omary anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano na baada ya mahojiano kukamilika, atafikishwa
mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake ambapo mwili wa marehemu umefanyiwa
uchunguzi wa Daktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za mazishi.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha
kunywa pombe kupita kiasi na kutokujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya kwani
ni vitendo ambavo vinashawishi kutenda matendo ambayo ni kinyume na sheria za
Nchi yakiwemo Ubakaji, wizi, (ukatili wa kijinsia na watoto) matendo ambayo yanaweza
kupelekea magonjwa na vifo.
Imeandaliwa na ;
KAMANDA
WA POLISI (M) SINGIDA
Toa maoni yako kupitia anwani zifuatazo;
Email : sylvestermac87@gmail.com,
: machibay.richard@yahoo.com
Sim no : 0768 367 454/0652683063
Facbook : mchibya richard/Sylvester Machibya
No comments