JAMBAZI
AUAWA NA WANANCHI MKOANI SINGIDA NA WENGINE WATATU WASHIKILIWA NA POLISI
KWA MAHOJANO.
Na Sylvester Richard.
SINGIDA;.
Jeshi la Polisi Mkoani
Singida linawashikilia watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi baada ya kutiliwa
mashaka na wananchi wakazi wa Kijiji cha Kitusha, Kata na Tarafa ya Kinampanda,
Wilayani Iramba.
Akiongea na
waandishi wa Habari katika ofisi ya RPC Singida leo, Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa ACP Simon S. Haule alieleza kuwa
mnamo tarehe 13.05.2016 majira ya saa 8:53 mchana Jeshi la Polisi Mkoani hapo
lilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Huko katika Kijiji cha Kitusha, kuna watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi
wameonekana Kijijini hapo na wanajihusisha na kushusha mizigo toka kwenye
magari ya mizigo yanayosafiri katika barabara kuu ya Singida – Nzega ambapo
baada ya Taarifa hizo, Askiri wa Jeshi hilo walienda moja kwa moja kwenye eneo
la tukio na Askari kwa kushirikiana na wanachi walifanikiwa kuwakamata
watuhumiwa wawili ambao ni Mathayo
Mathayo, (30), Mnyiramba mkazi wa Kitusha na Gedion Aron, (22), Mnyaturu Mkazi wa Maluga.
Wakati Askari
wakiwa kwenye msako wa kuwakamata wengine, walipata taarifa kwamba wananchi wamewakamata
watuhumiwa wengine wawili ambao ni Kess Yohana, (@ Mahope, (34), Mdengereko, Mkazi wa
Mvomero Morogoro, na Hassan ? @
Mjerumani, (35), Mlugulu, Mkazi wa Morogoro Mjini ndipo
askari walifika katika eneo la tukio na kukuta wananchi wakiwashambuli
watuhumiwa kwa silaha za jadi yakiwemo marungu, mawe na fimbo. Askari
walifanikiwa kuwatawanya wananchi na kuwaokoa watuhumiwa hao ambapo wakiwa
njiani kuelekea Hospitali, mtuhumiwa mmoja aitwaye Hassan ? @ Mjerumani alifariki dunia.
ACP Haule
alisema kuwa katika uchunguzi wa awali wa Polisi Mtuhumiwa Kess Yohana, (@
Mahope alikiri kuiba mali inayosafirishwa kwenye magari na wao ni wakazi wa
Morogoro na wamefika Mkoani Singida kwa Kazi ya Ujambazi.
Watuhumiwa
wamekutwa na mali mbalimabali inayodhaniwa kuwa ni ya wizi vikiwemo Robota la
nguo za mitumba, Compyuta moja ya mezani ( Desktop computer) naina ya Sonic na
Keyboard yake, Betri aina ya Tegger katoni 3, vifaa mbalimbali vya kuvunjia na
kujikinga miili yao wakati wakiruka kwenya magari yakiwa yanatebea na Nguo za
kufichia sura.
Kuhusiana na
tukio hilo watu watatu ambao ni Mathayo
s/o Mathayo, Gedion Aron na Kess Yohana
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano
na baada ya mahojiano kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili sheria
ichukue mkondo wake.
Kisha ACP Haule akatoa wito kwa watu
wanaojipatia mali kwa njia isiyo halali kuachana na vitendo hivyo bali wafanye
kazi halali zenya kuwapatia vipato halali. Pia viongozi wakiwemo mabalozi wa
Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji wanatakiwa kuyatumia vizuri
madaftari ya wageni kwa kuwasajili wageni wote wanaoingia katika himaya zao
ambapo itasaidia kutambua wageni wao kama ni raia wema au si wema na endapo
watamtilia mashaka mgeni yeyote watoe taarifa katika Kituo chochote cha Polisi
kilichopo karibu nao.
No comments