Mtu mmoja auawa
akifuatilia madeni yake Mkoani Singida, mwili wafichwa katika daraja, Kaimu Kamanda ACP Haule akemea vitendo vya Ukatili.
Hapo juu ni Picha ya Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida
ACP Simon S.Haule Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.
Na. Sylvester Richard
Singida,
Mtu mmoja anayejulikana
kwa Jina la William s/o Clement, (54), Mfanyabiashara wan a mkazi wa Ihanja aliuawa kwa kuchinjwa mbele na nyuma ya
shingo na Mtu/Watu wasiofahamika.
Akiongea na waandishi wa
habari leo Ofisini kwake, Kaimu Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Simon S. Haule alieza kuwa mwili wa marehemu uligundulika ukiwa
umefichwa katika daraja la Barabara ya Iseke
– Ihanja siku ya tarehe 23.06.2016 majira ya saa 1:30 asubuhi ambapo jeshi la
Polisi lilipewa taarifa.
Aidha ACP Haule alisema
kuwa baada ya kupata taarifa hizo timu ya wapelelezi Kutoka Jeshi la Polisi
ilitumwa kwenda kuchunguza chanzo cha mauaji hayo ambapo uchunguzi wa awali umebaini
chanzo cha mauaji hayo kuwa ni Deni la kiasi
cha Tshs. 400,000/= ambazo Marehemu alikuwa akimdai Hassan s/o Abdallah (38),
Mfanyabiashara wa Kijiji cha Mpetu.
Ailieleza uchunguzi umebaini
kuwa siku ya tarehe 22.06.2016 muda unaokadiriwa
kuwa saa 1:30 usiku Marehemu aliaga
nyumbani kwake kuwa anaenda kwa Hassan s/o Abdallah @ Msabo ambapo ilipofika majira ya saa 5:34 usiku
Marehemu alituma ujumbe wa simu ya mkononi kwa Mtoto wake Aitwaye Faraja s/o
Williamu, (23), Mkulima na mkazi wa Ihanja ikidai kuwa yeye anatoka kwa Msabo lakini kuna watu wanataka kumudhuru kwahiyo aende
amsaidie lakini kutokana na yeye kuwa usingizini alisoma ujumbe huo asubuhi
tarehe 23.06.2016 ndipo alipoanza kumpigia simu ambapo simu haikupatikana
hewani, aliamua kuwaarifu majirani nakuanza kumtafuta hadi hapo walipoukuta
mwili wake ukiwa umefichwa darajani.
Kufuatia tukio hilo ACP
Haule aliwaeleza waandishi kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia Hassan s/o
Abdallah @ Nsabo kwa mahojiano na baada
ya mahaojiano atafikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake ambapo Mwili
wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa Daktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa hatua
za mazishi.
Kisha Kaimu Kamanda
akatoa wito kwa wananchi wote na
kuwataka waachane na vitendo vya kikatili kama hivyo ambavyo viko kinyume na Sheria
za Nchi na dawa ya deni ni kulipa na siyo kutoa uhai wa mtu
ambaye hana hatia yeyote na kwa imani zao wanatakiwa kumrudia Mungu kwa kutenda
matendo yaliyo mema kwani yeye anaamini kuwa Madhebu mengi yanaamini kuwa kuua
ni dhambi kwa Mungu.
No comments