Watu wawili
wafariki dunia kwa kuangukiwa na Mgodi wakiwa wanachimba madini Mkoani Singida,
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
humo ACP Simon S. Haule awaonya
wachimbaji madini kuacha kuchimba bila kibali.
Hapo ni Picha ya Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida ACP Simon S. Haule akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake.
Na Sylvester
Richard.
Singida
Watu wawili wamefariki dunia Mkoani Singida wakiwa
wanapelekwa Hospitali ya Wilaya ya Iramba kwa matibabu baada ya kuporomokewa na mgodi wakiwa wanachimba
madini ya dhahabu katika mgodi wa Mbuyuni “B”
ulipo katika Kata ya Mgongo
Tarafa ya Shelui.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini
kwake Kaimu ACP Haule ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea siku
ya tarehe 19.06.2016 majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo aliwataja waliofariki
dunia kuwa ni pamoja na Mwidosi s/o Ramadhani, (44), na
Michael s/o George, (30), Wote Wanyiramba, Wakulima na wakazi wa Kijiji cha Mgongo.
Aidha ACP Haule alieleza kuwa Jeshi la
Polisi limefanya uchunguzi wa awali na kubaini
kuwa Eneo hilo la machimbo linamilikiwa na Kampuni inayojihusisha na uchimbaji madini ya BARICK
Kampuni ambayo ilimiliki eneo hilo kwaajili ya kufanyia utafiti wa madini mwaka
2006 na mpaka sasa halijaendelezwa
ambapo alitoa wito kwa wananchi kuacha kuchimba madini bila kibali
kutoka katika Wizara husika kwani Wizara ndiyo yenye wataalamu ambao wanaweza
kupima maeneo na kuruhusu kuendelea na shughuli za uchimbaji.
Kwa upende mwingine ACP Haule alieleza kuwa kuna ujali
mbili zimetokea Mkoani humo katika nyakati na maeneo tofauti ambapo ajali ya
kwanza ilitokea tarehe 19.06.2016 majira ya saa 9:15 alasiri huko katika Kijiji
cha Njilii, Kata , Tarafa na Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida , Barabara kuu
ya Singida – Dodoma ajali ambayo ilisababisha kifo na majeruhi ikishirikisha
Gari namba T.744 DFL TOYOTA HARRIER ikitokea
Mara kwenda Dar es salaam, ikiendeshwa na Bernad s/o Eprahim,(52) ambapo mtu
mmoja aitwaye Musa s/o Michael Mjaluo Miaka Mitatu Mkazi Wa Kitunda alifariki
dunia papo hapo na wengine watano kujeruhiwa.
ACP Haule aliwataja majeruhi kuwa ni Bernad s/o
Ephrahim Mjaluo Miaka 52 Mfanyabiashara Wa Kitunda Dsm Amepata Jeraha Kwenye
Paji La Uso Na Kuvunjika Mkono Wa Kushoto , Queenrose d/o Michael Mzanaki Miaka
Sita Mkazi Wa Ukonga Dsm, Amevunjika Mguu Wa Kushoto na Magreth d/o Bernad,
Mzanaki, Miaka 29, Mfanyabiashara Wa Dsm Amepata Maumivu Mwili Mzima. Wengine
ni Debora d/o Bernad, Mzanaki, Miaka, 43, Mfanyabiashara wa Dsm Amevunjika Mguu Wa Kushoto na Brayani d/o Idd, 03, Yrs ,
Mzanaki Wa Ukonga Ameumia Mwili Mzima na kuongeza kuwa majruhi wote wamelazwa katika
Hospitali Ya Wilaya Ya Manyoni na hali zao zinaendelea vizuri hali
kadhalika Mwili wa Marehemu umefanyiwa
uchunguzi Hospitalini hapo na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi. Alitaja Chanzo cha ajali ni
mwendo kasi na kutokuwa makini
barabarani ambapo Dereva Bernad s/o Eprahim anashikiliwa na Polisi kwa
uchunguzi kabla ya kufikishwa Mahakamani.
Kaimu Kamanda alieleza kuwa ajali ya pili ilitokea
tarehe 20.06.2016 majira ya saa 2:20 asubuhi
huko katika Mlima Saranda, barabara kuu ya Manyoni – Dodoma, Kata ya
Makutupora, Tarafa ya Kilimatinde, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida ambapo
gari namba T.145 AFA/T. 148 AFK SCANIA PULLING
likiwa linaendeshwa na Dereva
asiyefahamika akiwa na shehena ya marobota ya tumbaku akitokea Tabora
kwenda Morogoro lilipinduka na kuasababisha kifo cha Utingo wake aitwaye Saidi
s/o Mswagara, (33), Mkazi wa Tabora ambaye alifariki dunia papo hapo na kutaja
chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa Dereva kuendesha gari bovu ambalo
halikuwa na breki.
Kuhusiana na ajali hiyo, ACP Haule alisema
kuwa hakuna Mtu/Watu wanaoshikiliwa kutokana na Dereva wa Gari kutorokea
kusikojulikana baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo dereva huyo anatafutwa
ili akamatwe na kufikishwa Mhakamani ambapo alitoa wito kwa Madereva na
watumiaji wengine wa barabara kuzitumia barabara hizo kwa kuzingatia sheria,
kanuni na Taratibu za usalama barabarani.
No comments