DEREVA
MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI NA MMOJA ATOROKA BAADA YA KUSABABISHA AJALI
NA KUPELEKEA VIFO VYA ABIRIA 30 NA WENGINE 54 KUJERUHIWA MKOANI SINGIDA, KAMANDA
WA POLISI MKOA ACP THOBIAS G.SEDOYEKA
AELEZEA JINSI AJALI ILIVYOTOKEA.
simu No. 0768 367454
0652 683063
Facebook. Machibya Richard.
Hapo juu ni picha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Thobias G. Sedoyeka akisikiliza kwa makini hoja iliyokuwa ikitolewa na mmoja wa waandishi wa habari ofisini kwake.
Na
Sylvester Richard
Singida.
Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Thobias G. Sedoyeka
amebainisha chanzo cha ajali ya magari mawili yiliyogongana uso kwa uso na
kusababisha vifo na majeruhi.
Akiongea na
waandishi wa habari jana Ofisini kwake majira ya saa 5:45 mchana, ACP Thobias
Sedoyeka alieleza kuwa Mnamo tarehe
04/07/2016 majira ya saa 8:15 mchana huko Kijiji cha Maweni, Kata ya Ngumiti,
Tarafa ya Kintinku, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida, Gari No. T.247 BCD
SCANIA BUS ikitokea Kahama kuelekea Dar
es salaam ikiendeshwa na Jeremiah s/o Martin Sempungwe
(?) aligongana na Gari No. T. 531 DCE
SCANIA BUS likitokea Dar es salaam
kwenda Kahama likiendeshwa na Boniface s/o Mwakalukwa na kusababisha vifo vya
abiria (30) Wanaume (21) na wanawake
(09) miongoni mwao watoto (05) ambao
bado hawajatambuliwa na kusababisha majeruhi kwa abiria (54) kati ya hao wanawake (20) na wanaume
(30) miongoni mwao watoto ni (04) ambapo
majeruhi waliotambuliwa ni (48).
Kamanda
Sedoyeka alisema kuwa Majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Manyoni na Dodoma huku hali zao zikiendelea vizuri, hali kadhalika
miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni na
hospitali ya Mkoa wa Dodoma
ikisubiri kutambuliwa na hatimaye kukabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za Mazishi.
ACP Sedoyeka alibainisha Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa madereva wote wawili, ambapo
walipofika katika eneo la Maweni
madereva wote walionyeshana ishara ya kuwasiliana kwa kuwashiana taa za gari na
kila mmoja Kuhama kutoka upande mmoja kwenda mwingine na hivyo kupelekea kushindwa kuyamudu
magari hayo na kusababisha ajali hiyo. Dereva Jeremiah s/o Martin (34) ,Mgogo,
mkazi wa Dar es salaam
mwenye gari No. T. 247 BCD amekamatwa na Dereva
Boniface Mwakalukwa mwenye gari No. T. 531 DCE ametoroka baada ya ajali
kutokea , Juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea.
Kamanda
Sedoyeka hakusita kutoa wito kwa Madereva
na watumiaji wengine wa barabara ambapo
aliwataka kuzitumia barabara hizo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za
Usalama barabarani na kuongezea kwa kusema kuwa Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali mwananchi /
Dereva yoyote atakayevunja sheria za usalama barabarani pindi wanapotumia
barabara hizo.
No comments