Breaking News




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli atuma rambairambi kwa familia za waliofariki dunia kwa ajali Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambiambi kwa familia za watu 29 waliofariki dunia papo hapo baada ya   ajali kutokea ikishirikisha Mabasi mawili yanayomilikiwa na Kamuni ya City Boys iliyotokea tarehe 04.07.2016 majira ya saa 8:45 mchana katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Mhandisi Methew Mtigumwe muda mfupi tu baada ya kupokea taarifa za ajali hiyo mbaya na kuelezea masikitiko yake juu ya kutokea kwa ajali hiyo.

No comments