Breaking News

Jeshi la Polisi Mkoani Singida la fanya mazoezi yake ya utayari katika Manispaa ya Mji huo. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo  awaonya  watakaojihusisha na UKUTA.


Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida wamefanya mazoezi ya utayari katika Manispaa ya Singida. Akiongea na waandishi wa habari katika Uwanja wa Mikutano uliopo maeneo ya Mandewa, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Mayalla Towo amesema kuwa mazoezi hayo yamefanyika leo tarehe 22.08.2016 kuanzia majira ya saa 3:00 - 5:15 asubuhi.

Kamanda Towo ameyataja mazoezi hayo kuwa ni mazoezi ya  kawaida ambayo hufanyika mara kwa mara ili kuwaweka askari kuwa tayari kwa lolote linaloweza kutokea na kuleta uvunjifu wa amani. 

Amesema mazoezi hayo mara nyingi hufaynika alfajiri ambapo wananchi wengi wanakuwa bado wamelala lakini kwa kipindi hiki mazoezi yamefanyika mchana ili wananchi wajionee wenyewe kwani askari wameajiriwa kwa ajiri ya kuwalinda wao na mali zao kwahiyo nivizuri kujua Jeshi lao lina muonekano gani na wao kujisikia kuwa wanalindwa na wanaishi  kwa amani.

Akizungumzia suala la Maandamano ya kikundi kilichoundwa na Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinachojulikana kwa jina la UKUTA,  Kaimu Kamanda aliwataka wananchi wasijihusishe na suala hilo na wala wasijitokeze kwani halipo kisheria na endapo  atajitokeza mtu yeyote kushiriki  asimlalamikie mtu kwani sheria itachukua mkondo wake.













No comments