Angalia hapa picha za mchezo wa kupimana nguvu kati ya Timu ya Mwadui FC ya Shinyanga na Timu ya Singida Unitedi ya Singida. Mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Namfua uliopo katika Manispaa ya Singida siku ya Tarehe 20.08.2016 majijira ya saa 10:30 Jioni huku timu zote zikitoka sare ye bao moja kwa moja katika dakika 92 za mchezo huo.
Waamuzi wa pambano kati ya Timu ya Mwadui FC na Singida United wakiwa na manahodha wa timu zote mbili muda mfupi kabla ya pambano hilo kuaanza. Watatu kutoka kulia ni Shabani Msangi ambaye ndiye mwamuzi wa kati wa pambano hilo.
Wachezaji wa Timu ya Singida United wakiwakaribisha wachezaji wa Timu ya Mwadui FC tayari kwa mchezo wa kupimana nguvu katika uwanja wa Namfua uliopo katika Manispaa ya Singida.
Wachezaji wa Timu ya Mwadui FC ya Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa kupimana nguvu na timu ya Singida United Katika uwanja wa Namfua Manispaa ya Singida.
Wachezaji
wa Timu ya Singida United wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi
kabla ya kuanza kwa mchezo wa kupimana nguvu na timu ya Mwadui FC ya Shinyanga
Katika uwanja wa Namfua Manispaa ya Singida
Mchezaji wa Timu ya Singida United akimpiga chenga Mchezaji wa Timu ya Mwadui FC katika mchezo wa kupimana nguvu Katika uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida
Mchezaji wa Timu ya Mwadu FC akimpiga chenga Mchezaji wa Timu ya Singida United katika mchezo wa kupimana nguvu Katika uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida
Mchezaji wa Timu ya Singida United akiwa amelala chini baada ya kufanyiwa madhambi na Mchezaji wa Timu ya Mwadui FC katika mchezo wa kupimana nguvu Katika uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida
No comments