FIESTA, FIESTA, FIESTA KUUTIKISA MJI WA SINGIDA SEPTEMBER 11 2016.
Jeshi la Polisi lajipanga vizuri katika kuimarisha ulinzi na usalama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina msaidizi mwandamizi
wa Polisi (SACP) Peter c. Kakamba
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina msaidizi mwandamizi
wa Polisi (SACP) Peter c. Kakamba akiongea na Timu ya waandishi wa habari kutoka Clouds Media Ofisini kwake.
Kampuni ya Cluods Intertainmet yenye
makao yake Makuu Jijini Dar es salaam kwa kushirikiana na Prime time Promotions
inatarajia kufanya tamasha linalojulikana kwa jina la FIESTA Mkoani Singida
siku ya tarehe 11.09.2016 kuanzia majira ya saa 11:00 jioni katika Uwanja wa
Namfua uliopo katika Manispaa ya Singida.
Akiongea na waandishi wa habari
ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina msaidizi mwandamizi
wa Polisi (SACP) Peter c. Kakamba amesema kuwa kutokana na Tamasha hilo, Jeshi
la Polisi Mkoani humo limejipanga vyema kuimarisha ulinzi na usalama katika
uwanja wa Namfua pamoja na maeneo
mengine ya Mji huo kwa ujumla ili kuhakikisha FIESTA hiyo inafanyika kwa amani
na utulivu.
Aidha Kamanda Kakamba alieleza kuwa
hali ya usalama Mkoani Singida inaridhisha kwani vitendo vya kihalifu kwa
ujumla vimepungua kwa kiasi kikubwa na kutoa wito kwa wananchi wa Singida
kushiriki tamasha hilo kwa amani na utulivu bila kuvunja sheria za Nchi.
Aliwataka pia madereva wa vyombo vya usafiri kuendesha vyombo vyao kwa
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepusha ajali
zisizotarajiwa.
Kamanda hakusita kuwaasa Raia wema kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa
kutoa taarifa za uhalifu/wahalifu ili hatua stahiki zichukuliwe.
Kama una habari, maoni, ushauri, picha, na matangazo wasiliana nasi kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Facebook
whats app 0768 367454 .
No comments