Wakati wiki yanenda kwa usalama ikizinduliwa Kitaifa Mkoani Geita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida
afunga mafunzo ya usalama barabarani kwa wapanda pikipki (boaboda ) 108 yalifadhiliwa na APEC. Katika Kijiji cha Mtunduru Singida.
APEC (Anti Porverty and Environmental Care) Ni shirika
lisilokuwa la kiserikali ambalo
lilianzishwa mwaka 2012 Nchini Tanzania na makao yake makuu yapo Jijini Dar es salaam. Tangu
kuanzishwa kwa shirika hilo na kwa
ushirikiano mkubwa na Jeshi la Polisi Tanzania, limekuwa likijishughulisha na
ufadhili wa mafunzo ya Usalama barabarani, Ujasiliamali na ushirikishwaji kwa
madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda. Mkoani Singida Shirika hilo
lilianza kutoa mafunzo mwaka 2013 ambapo mpaka kufikia Septemba 2016 Shirika
limeweza kutoa mafunzo katika Tarafa zote za Mkoa wa huo.
Aidha APEC imeweza kuendesha mafunzo yaliyochukua muda
wa wiki mbili katika Tarafa ya Sepuka, Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida kwa
madereva wa pikipiki (boaboda) 108 mafunzo ambayo yalifunguliwa tarehe
13.09.2016 na kufungwa rasmi tarehe 26.09.2016 siku ambayo wiki ya nenda kwa
usalama Kitaifa ilizinduliwa Mkoani Geita.
Aidha mafunzo hayo yamefungwa na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Singida Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Peter C. Kakamba
ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo.
Akiongea na wahitimu wa mafunzo katika hafla hiyo
iliyofanyika katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT lilipo katika Kijiji na Kata ya
Mtunduru, Mgeni Rasmi ametoa pongezi kwa Shirika la APEC kwa kufadhili mafunzo hayo ambayo yanalenga
kuwajengea walengwa uwezo wa kutambua sheria za usalama barabarani hali ambayo
imepunguza ajali kwa kiwango kikubwa kwa mujibu wa takwimu iliyosomwa na
Mratibu wa mafunzo hayo Mkaguzi wa Polisi Iddah Ringo takwimu ambayo ilieleza
kuwa mwaka 2014 katika Mkoa wa Singida kulikuwa na ajali 4 zilizosababisha vifo
kwa siku ambapo baada ya mafunzo hayo kuanza kutolewa mwaka 2015 ajali zilipungua na kufikia ajali
15 tu kwa mwaka
Kamanda aliwapongeza madereva wote waliohudhuria
mafunzo hayo na kuwataka kuendesha
vyombo vyao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa kuwa tayari
wameshafundishwa na wanazielewa vizuri kitendo ambacho kitawasaidia kuepuka
ajali zisizo za lazima huku akiwataka kuendesha vyombo vyao kwa kujihami. Akachukua
nafasi hiyo kuwaomba watu wote wakiwemo
watumishi wa Serikali bila kujali
jinsia zao kushiriki katika mafunzo hayo
na ikiwezekana wawe walimu kwa wengine.
Akizungumzia suala la kujichukulia sheria mkononi,
Kamanda aliwaasa kuachana na suaala hilo
kwani linaweza kusababisha madhara makubwa yakiwemo kujeruhi na hata wakati mwingine
vifo. Aliwaomba watoe taarifa za wahalifu/uhalifu katika vituo vya Polisi
vilivyokaribu na wao au kwa viongozi wa Serikali ili matatizo yao yashughulikiwe kisheria.
Naye Mkurugenzi wa APEC Tanzania Respicius Bingire
Timanywa alitumia nafasi hiyo kuliomba Jeshi la Polisi kubadili mfumo wa
kufanya oparesheni za wamiliki wa pikipiki ambao hawalipii ushuru pikipiki zao
barabarani bali wawatumie Watendaji wa Vijiji/Kata katika kuwabaini wamiliki wa
vyombo vya usafiri kwani wao ndio wanafahamu. Pia aliwaomba TANROADS kuweka
vibao vinavyonesha alama za usalama barabarani yakiwemo matuta, madaraja,
miteremko, na kona kali katika barabara za vijijini kwani barabara nyingi
hazina alama hizo ambazo humsaidia dereva kujua nini kilichoko mbele yake na
hivyo kuchukua tahadhali.
Kutokana na mafunzo hayo, wananchi wengi wametambua
kuwa udereva wa pipiki (bodaboda) ni sehemu ya ajira na kimekuwa ni chanzo
kikubwa cha mapato kwa vijana wengi Nchini Tanzania hali ambayo imechangia kwa
kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa wafungwa magerzani amesema Mkurugenzi
Timanywa. Hivyo ameliomba Jeshi la Magereza Nchini kushirikiana na shirika hilo kwa kutoa elimu ya ujasiliamali kwa kuwa yeye
anatambua kuwa Jeshi hilo lina wataalamu wa
kutosha kufanya jukumu hilo.
Zifuatazo ni picha za hafla ya kufunga mafunzo ya Usalama barabarani, Ujasiliamali na
ushirikishwaji Katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT Katika Kijiji na Kata ya
Mtunduru, Tarafa ya Sepuka, Wilyaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Peter C. Kakamba akihotubia wahitimu wa mafunzo ya Usalama barabarani, Ujasiliamali na ushirikishwaji Katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT Katika Kijiji na Kata ya Mtunduru, Tarafa ya Sepuka, Wilyaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Wapili kutoka kushoto aliyesimama ni Mkurugenzi wa APEK Tanzania Respicius Bingire
Timanywa akisisitiza jambo katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya Usalama barabarani,
Ujasiliamali na ushirikishwaji kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) Katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT Katika
Kijiji na Kata ya Mtunduru, Tarafa ya Sepuka, Wilyaya ya Ikungi Mkoani
Singida.
Wakwanza kulia ni Mratibu wa Mafunzo ya Usalama barabarani, Ujasiliamali na ushirikishwaji kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) Mkoa wa Singida Mkaguzi wa Polisi Iddah Ringo akisisiza jambo Katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT Katika Kijiji na Kata ya Mtunduru, Tarafa ya Sepuka, Wilyaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya Usalama barabarani,
Ujasiliamali na ushirikishwaji kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) wakiwa katika hafla fupi ya kufunga mafunzo katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT Katika
Kijiji na Kata ya Mtunduru, Tarafa ya Sepuka, Wilyaya ya Ikungi Mkoani
Singida.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Singida Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Peter C. Kakamba akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Usalama barabarani, Ujasiliamali na
ushirikishwaji nje ya Ukumbi wa Kanisa la KKKT Katika Kijiji na Kata ya
Mtunduru, Tarafa ya Sepuka, Wilyaya ya Ikungi, Mkoani Singida.
Katikati ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya Usalama barabarani,
Ujasiliamali na ushirikishwaji kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) muda mfupi baada ya hafla fupi ya kufunga mafunzo nje ya Ukumbi wa Kanisa la KKKT Katika
Kijiji na Kata ya Mtunduru, Tarafa ya Sepuka, Wilyaya ya Ikungi Mkoani
Singida.
No comments