Dr. Nchimbi awaongoza watumishi wa uma katika kufanya
mazoezi ya viungo Mkoani Singida.
Na Sylvester Richard
Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi amewaongoza
watumishi wa uma waliopo katika Manispaa ya Singida katika kufanya mazoezi ya
viungo vya mwili.
Aidha mazoezi hayo yameanza kwa kukimbia kutoka katika
Ofisi za Manispaa ya Singida hadi viwanja vya michezo vya Shule ya Sekondari
Kindia ambapo mazoezi mengine yamefanyika.
Baada ya mazoezi hayo, Dr. Nchimbi akachukua nafasi
kuwashukuru na kuwahamasisha watumishi wa Uma waliofika katika mazoezi hayo
kujijengea tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuiweka miili yao tayari
kwa jambo lolote kwani mazoezi huleta afya njema na kuwataka wasije katika
mazoezi kwa sababu ya maelekezo kutoka juu.
Hata hivyo Dr. Nchimbi amewaahidi watumishi wa Uma na
wananchi kwa ujumla kuwa kila wiki ya pili ya mazoezi ya kila mwezi itakuwa nifursa kweke kutoa taarifa ya
maendeleo ya Mkoa ambapo amewaeleza
wananchi wa Singida kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta ambalo linatoka Nchini Uganda
kwenda Tanga kuwa litapiata Mkoani
Singida na Timu ya wataalamu ambo wanakuja kutambulisha maeneo yatakayopitiwa na
bomba hilo tayari wameshafika Mkoani Singida.
Akatanabaisha kuwa, Kutokana na kupita kwa Bomba hilo
Mkoa wa Singida unatarajia kunufaika nalo kwa kiasi kikubwa kwani wananchi wa
Singida watajipatia ajira mbalimbali na kuongeza thamani ya Uchumi wa Singida
na Nchi yote kwa ujumla.
Mwisho Dr. Nchimbi aliwataka wananchi wote wa Mkoa huo
kushiriki mazoezi hayo na kuyafanya kuwa ni sehemu ya maisha yao kuliko kusubiri
siku ya Juma mosi ya pili ya mwezi na kwa mazoezi hayo watakuwa na afya njema ambayo ndiyo itakayowapa fursa mbalimbali zitakazoletwa na Serikali ya awamu
ya tano ya Dr. John Joseph Pombe Magufuli zitakazohusisha Mkoa wa Singida.
Mbele pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi akiongoza watumishi wa uma waliopo Manispaa ya Singida
kwa kutoa mfano wa mazoezi kama anavyonekana pichani katika viwanja vya Shule
ya Secondari Kindai.
Pichani ni Katibu tawala
Mkoa wa Singida Dr. Anjelina Lutambi akishiriki
mazoezi kwa kucheza mchezo ujulikanao kama mchezo wa kumkamata panya ambapo yeye
ndiye anayetakiwa amkamate mwenzake aliyeko mbele.
Mbele pichani katikati mwenye kofia nyeupe ni Mkuu wa
Wilaya ya Singida Mh. Elias John Tarimo akiungana na watumishi wengine kufanya
mazoezi katika viwanja vya Shule ya
Secondari Kindai.
Katikati mwenye traki yenye rangi ya bluu nyeusi yenye michirizi myeupe na mmoja mwekundu ni SSP Florence Menda OCD Wilaya ya Singida akishiriki mazoezi kwa
hamasa kubwa kwa kukimbia mchaka mchaka ulioanzia Ofisi za Manispaa ya Singida
hadi Shule ya Secondari Kindai.
Watumishi wa Uma Mchanganyiko wakishirika mazoezi ya
viungo baada kukimbia mchaka mchaka kutoka Ofisi za Manispaa ya Singida hadi
viwanja vya michezo Shule ya Secondari Kindai.
Kama una habari, Matangazo, Picha, Maoni na Ushauri. Wasiliana nasi kwa anwani zifuatazo
E - mail - sylvestermac87@gmail.com
- machibya.richard@yahoo.com
Sim No. - 0768 367 454 / 0652 683 063
Facebook Machibya Richard
No comments