Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Isaya K. Mbughi. akiongea na waandishi wa habari.
Jeshi la polisi Mkoani Singida
linawashikilia wafanyabiashara wawili ambao ni John Shirima @ John Ngozi na Jamesi Michael Poul
baada ya kupatikana na pombe
iliyofungashwa kwenye mifuko ya plastiki
maarufu kwa jina la viroba aina mbalimbali kiasi cha katoni 2690.
Akiongea na waandishi wa habari baada
ya ukamataji huo siku ya tarehe
10.03.2017 majira ya 10:30 jioni Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu
mwandamizi (SSP) Isaya Mbughi ameeleza kuwa
Wafanyabiashara hao ambao ni wakazi wa manispaa ya Singida wanashikiliwa
na Jeshi hilo baada ya kukutwa na viroba hivyo vikiwa vimehifadhiwa kwenye stoo
huku wakitambua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Aidha Kaimu Kamanda ameeleza kuwa
viroba hivyo vimepatikana kutokana na opareshini ya kukomesha biashara ya
madawa ya kulevya na pombe inayofungahswa katika mifuko ya plastiki
(viroba ) ambapo Jeshi la Polisi
likishirikiana na Afisa biashara , Afisa afya na Afisa madhingira
Manispaa ya Singida walifanikiwa kubani uwepo wa pombe hiyo ya viroba katika
stoo mbili moja iliyopo maeneo ya Soko kuu na nyingine iliyopo Maeneo ya
Karakana zinazomilikiwa na wafanyabiashara hao wawili .
Watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa
na Polisi kwa mahojiano ili kubaini sababu za kumiliki pombe hizo ambazo zimepigwa marufuku hapa Nchini na
endapo watabainika kuwa na hatia watafikishwa mahakamani Kujibu tuhuma
zinazowakabili.
SSP Mbughi ametoa wito kwa wananchi
wote kuacha kujihusisha na uuzaji na utumiaji wa pombe hizo za viroba na madawa
ya kulevya kwani zimepigwa marufuku na
Serikali na endapo watabainika kufanya hivyo watakamatwa na sheria itachukua
mkondo wake.
Afisa Biashara Manispaa ya Singida
Ndughu Desmond D. Muna ameeleza kuwa katika stoo zote mbili kuna shehena ya
viroba yenye thamani inayokadiriwa kuwa
na kiasi cha zaidi ya Tsh. Milion 2. ambapo amewataka wafanyabiashara wote ambao
bado wanavificha viroba wavisalimishe
mara moja kuliko kusubiri mpaka wakamatwe kwani oparesheni hiyo ni endelevu
kutokana na Serikali kupiga marufuku
biashara hiyo.
Naye mfanya biashara mmoja Jamesi Michael ambaye ni mmiliki wa Stoo iliyopo
maeneo ya Karakana ijulikanayo kwa jina la Kiomboi General Store ameeleza kuwa
yeye aliacha kuuza viroba hivyo tangu tamko la Serikali lilipotolewa isipokuwa aliiweka hapo stoo ili kusubiri tamko la
serikali juu ya viroba hivyo huku akichelewa kivisalimisha kutokana na yeye
kuwa safarini. Hata hivyo emechukua nafasi hiyo kuiomba Serikali iangalie iweze
kuwongezea muda ili waweze kuuza bidhaa hiyo iliyopo ili warudishe gharama walizonunulia
kiwandani.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Isaya K. Mbughi akionyesha pombe ya viroba iliyopigwa marufuku katika moja ya stoo iliyoko Maspaa ya Singida.
Mbele pichani ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Isaya K. Mbughi akionyesha pombe ya viroba iliyokamatwa.
Katika picha ni pombe ya viroba iliyopigwa marufuka hapa Nchini.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Isaya K. Mbughi akiwasili katika moja ya Stoo iliyohifadhi pombe ya viroba iliypo katika maeneo ya Karakana Manispaa ya Singida.
Kama una
maoni, habari, Matangazo na picha
wasiliana nasi kupitia anwani zifuatazo;
E-mail
sylvestermac87@gmail.com
Facebook
Machibya Richard.
SIM No. 0768 367454/ 0652 683063
No comments