Breaking News


ONYO KALI KWA WAUZA PEMBEJEO FEKI,
 HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WATAKAOBAINIKA.



SINGIDA
Wauzaji wa pembejeo ambao sio waaminifu wamepewa onyo kali na endapo atabainika yeyote anayewalaghai wakulima na kuwauzia pembejeo ambazo sio halali hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.


Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji ametoa onyo hilo wakati akizindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana na shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa alizeti Mkoani Singida ili kulima zao hilo kibiashara zaidi.


Chowaji amesema kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya wakulima ambao hukumbana na wauzaji wa pembejeo ambao sio waaminifu na kuwalaghai kwakuwa wakulima hao hawana elimu na uelewa hasa wa viuatilifu au mbegu ambazo ni halisi.


Ameongeza kuwa mkono wa serikali ni merfu na utawabaini popote walipo hivyo waache mara moja kwani kwa kufanya hivyo wanakirudisha nyuma kilimo cha alizeti ambacho ni tegemeo kwa ajili ya uchumi wa viwanda Mkoani Singida.


Singida tuna Viwanda vya kuamua mafuta ya alizeti vikubwa viwili, vya kati vitatu na vidogo 115 na kufanya jumla ya viwanda vya alizeti kuwa 120, vyote hivyo vinategemea alizeti ya mkulima, lakini pia mkulima anakuwa na matarajioa makubwa, hao wauzaji pembejeo wasio waaminifu hatutawavumilia, tena waache mara moja”, amesisitiza Chowaji.


Aidha amelipongeza shirika la AMDT kupitia mradi wa Faida mali kwa kuuchagua Mkoa wa Singida ili kuboresha kilimo cha alizeti hasa kwa ajili ya mkulima mdogo.


Chowaji amesema viwanda vya alizeti Mkoani Singida hufanya kazi kwa miezi minane kwa mwaka badala ya mwaka mzima kutokana na kuwa alizeti inayozalisha bado haitosheleshi viwanda hivyo kufanya kazi mwaka mzima.


Amesema matumaini makubwa ya serikali mkoani hapa ni kuwa mradi huo utasaidia kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kuifanya Singida ya Viwanda kuwa bora zaidi pamoja na kuliboresha zao lenyewe la alizeti kwa kutumia pembejeo za kisasa zaidi.


Chowaji amewataka wakulima wote wa alizeti kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga katika vikundi ili waweze kufikiwa kwa urahisi na kunufaika, pia waache kilimo cha mazoea kwakuwa alizeti ni biashara kubwa ambayo itawakomboa kiuchumi na kukupa pato la mkoa wa Singida.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la AMDT Michael Kayombo amesema shirika hilo kupitia Mradi wa Faida mali utahakikisha unasaidia upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo wa alizeti Mkoani singida.


Kayombo ameongeza kuwa mradi utaboresha huduma za ugani kwa kutoa taarifa sahihi na mapema juu ya kilimo cha alizeti kwa wakulima na taarifa hizo zitatolewa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno hivyo kuwafikia mapema.


Amreongeza kuwa watahakikisha wakulima wanapata soko la uhakika la zao hilo ndani na nje ya mkoa wa singida pamoja na kuhakikisha bei ya zao hilo ni yenye kumnufaisha mkulima na sio kumdidimiza zaidi.


Naye Mtendaji Mkuu wa Chama cha wasindikaji wa Mbegu za alizeti Tanzania Daud Musa Mwasantaja amesema viwanda vya alizeti bado vina uhitaji mkubwa wa alizeti kwa kuwa viwanda vyao vimekuwa vikiendeshwa chini ya malengo kutokana na mbegu hizo kuwa chache.


Mwasantaja amesema wana imani kuwa mraadi wa Faida Mali utasaidia kuongeza uzalishaji wa alizeti hivyo kuwasaidia kuongeza pia uzalishaji katika viwanda vyao.


Ameongeza kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha na hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi walime zao hilo kwa wingi watapata wateja na kwa bei ambayo ni nzuri.


Nao wakulima walioshiriki uzinduzi wa maradi huo wamesema mradi huo umekuja muda muafaka kwakuwa na wao wanatamani kupata faida kutokana na kilimo hicho kwakuwa baadhi bado wanalima kwa mazoea na kwa kutumia mbegu ambazo hazizalishi kwa wingi.









Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji akisoma bango mara baaa ya kuzindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana na shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida.
 


Mkurugenzi wa Shirika la AMDT Michael Kayombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.



 Baadhi ya wadau waliohudhuruia uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.




Mkurugenzi wa mradi wa Faida Mali mkoa wa Singida Tom Silayo akisoma taarifa ya mradi huo kwa wajumbe waliohudhuria uzinduzi wa mradi utakaowasaidia wakulima kulima alizeti kibiashara.



Mtendaji Mkuu wa Chama cha wasindikaji wa Mbegu za alizeti Tanzania Daud Musa Mwasantaja akiwahakikishia wakulima wa alizeti upatikanaji wa soko katika uzinduzi wa Mradi wa Faida Mali.

Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E- mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . Whats app 0629655814
  

No comments