Breaking News




Zaidi ya hekari 20 kutengwa Mkoani Singida ili kujenga kituo kikubwa cha Olympic.




Na. Sylvester Richard.

SINGIDA
Mkoa wa Singida unatarajia kutenga eneo lenye ukubwa zaidi ya Hekari 20 kwa ajiri ya kujenga kituo kikubwa cha Olympic  Africa.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkuu wa Mko wa Singida Dr. Rehema Nchimbi wakati akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya Olympic Duniani siku ya tarehe 25.06.2017 maeneo ya viwanja vya People’s katika Manispaa ya Singida Kitaifa. Hata hivyo maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka tarehe 23 Juni ambapo kutokana na siku hiyo kuwa ni siku ya kazi Nchini Tanzania , Tamasha hilo lilihamishiwa siku ya tarehe 25 kwa kuwa ni siku ya mapumziko.

Aidha Dr. Nchimbi amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Singida kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki Tamasha hilo ambapo washiriki zaidi ya 800 wameshiriki na kupata vyeti kwa makundi na kwa mshiriki mmoja mmoja kwa kutegemea na ushiriki wake.

Hata hivyo Dr. Nchimbi ameishukuru Kamati Tendaji ya Olympic Tanzania ambayo imeongozwa na Makamu wa Raisi Olympic Tanzania Ndugu Henery Tandao kwa kuamua Tamashama hilo kufanyika Mkoani Singida na Kuwakaribisha waje Kujenga Makao Makuu ya Olympic Tanzania Singida kwa kuwa ni jirani na Makao Makuu ya Nchi ambayo yapo katika Mkoa wa Dodoma. 

Aliwaomba waweke kumbu kumbu ya washiriki walioshiriki na kushinda ili Orodha hiyo iandaliwe vizuri na kuwakilisha katika mbio mbalimbali hapa Nchini na kwingineko Duniani. 

Dr. Nchimbi amechukua nafasi kuwashukuru Wanamichezo/Wanariadha ambao wameweza kuiletea Nchi ya Tanzani Medani mbalimbali kutoka Mataifa mbalimbali Duniani na hivyo kuipa Heshima kubwa Nchi hiyo kutokana na ushindi wao ambapo ameupongeza Mkoa wa Singida kwa kujitahidi kutoa wanariadha waengi wanaoiwakilisha Nchi ya Tanzania katika Mashindano ya Kimataifa. 

Ametaja baadhi ya wanariadha mahiri walioliinua Taifa katika Riadha  kuwa ni pamoja na Selina Zacharia, Juma Nyampanda,  Anthon Mwingereza, Hawa Huseni, Ally Nyonyi, Christopher Isegwe, na Zakia Mrisho Mohamed. Wengine ni Juma Makula na Alfonce Felix Simbu.

Mgeni Rasmi aliiahidi Kamati ya Olympiki kushirikiana nayo bega kwa bega kwa kusikiliza shida zao kupitia Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Mkoa wa Singida ambaye Afisa Tawala Mkoa Mh. Anjelina Lutambi na kuomba Tamasha hilo lifanyike tena Mkoani Humo kwa mwaka ujao kwani wananchi wa Singida wako tayari na kuwasisitiza waje wenyewe na waweke Makao makuu ya Olympic Singida.

Naye Filbert Bay Katibu Mkuu Kamati ya Olympic alieleza lengo la kufanya tamasha hilo kuwa ni utamaduni ambao umejengeka tangu mwaka 1894 wakati  Kamati ya Olympic inaanzishwa na kuamua tarehe 23. Juni ya kila mwaka kufanya maadhimisho ambapo Nchi zaidi ya 200 Duniani huadhimisha kwa lengo la kuhamasisha kuinua na kuimarisha michezo mbalimbli ikiwemo Riadha, Mpira wa miguu, Mpira wa Kikapu na michezo mingine.

 Mh. Bay Amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa Ahadi ya kutoa eneo la kujenga kituo cha Olympic Singida kwani wataweza kujenga viwanja vya michezo mbalimbali pamoja  na kumbi za mikutano ambapo vipaji mbalimbali vitaibuliwa.


  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi akishiri Tamasha la Olympic pamoja na Washiriki wenye umri mdogo na mmoja mwenye umri Mkubwa kuliko wote katika viwanja vya People's Manispaa ya Singida.
 


 Mkuu wa Moa wa Singida Dr. rahema Nchimbi akikabidhi zawadi kwa Bibi Tecla Mwangu mwenye umri wa miaka 97 Mkazi wa Manispaa ya Singida na Mshiri wa Tamasha la Olympic mwenye umri mkubwa kuliko washiriki wote yeye alipata zawadi ya Tsh. 30,000/=
 

  Mkuu wa Moa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi akikabidhi za wadi kwa Mtoto Nadhifu Hassani Mshiriki wa Tamasha la Olympic mwenye umri wa miaka 4 na ndiye mwenye umri mdogo  kuliko washiriki wote yeye alipata zawadi ya Tsh. 10,000/=

 
Mkuu wa Moa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi akikabidhi za wadi kwa Mtoto Karen Nsasu, (6), Mshiriki wa Tamasha la Olympic ambaye amepata zawadi maalumu ya ushiriki kiasi cha Tsh. 50,000/=



Katikati aliyeshika kitambaa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi akishangilia siku ya Olympic na watoto wa Singida.



 Pichani ni Katibu Mkuu wa Olympic Taifa Ndugu Filbert Bay akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Tamasha la Olympic kumalizika katika viwanja vya People's  Manispaa ya Singida.





 Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E- mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . Whats app 0629655814






No comments