Jeshi la Polisi Mkoani Singida, lafanikiwa kupunguza ajali za barabarani kutoka ajali 69 kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi kufikia ajali 24.
Jeshi la Polisi Mkoani Singida, lafanikiwa kupunguza ajali za barabarani kutoka ajali 69 kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi kufikia ajali 24.
SINGIDA.
Jeshi la Polisi Mkoani
Singida, limefanikiwa kupunguza ajali za barabarani kutoka ajali 69 kwa kipindi
cha mwaka 2016 hadi kufikia ajali 24 katika kipindi cha mwezi Januari mpaka
Juni mwaka huu.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa
wiki na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Debora Magilingimba wakati
akitoa taarifa ya uhalifu kwa Mkoa wa Singida ambapo amesema katika ajali hizo
24 zilisababisha vifo vya watu 29 na hapajakuwepo majeruhi kabisa.
ACP Magiligimba amesema kupungua
kwa ajali kumetokana na Jeshi hilo kutoa elimu ya usalama barabarani mara kwa
mara hasa katika maeneo ya vijijini, mitaani na hata katika mafunzo ya udereva.
Ameongeza kuwa jeshi hilo
limekuwa likithibiti mwendo kasi katika barabara kuu, kuthibiti ulevi kwa
upimaji wa kilevi kwa madereva wote wa vyombo vya usafiri na hivyo kupelekea
ajali kupungua sana kwa Mkoa wa Singida.
“Pia tumeendelea kutoa
elimu ya usalama barabarani mashuleni, vyuoni na katika nyumba za ibada. Lengo
ni kuiongozea jamii uelewa zaidi unaohusu masuala yote ya ulinzi na usalama, na
sheria za usalama barabarani”, amefafanua.
Aidha, ACP Magiligimba amesema
makosa madogo yamepungua kwa asilimia 0.8 ambapo jumla ya makosa madogo 22,222
yameripotiwa katika kipindi cha januari hadi juni mwaka huu, ikilinganishwa na
makosa kama hayo 22,403 yaliyotokea kipindi kama hicho mwaka jana.
“Katika makosa hayo madogo,
jumla ya wakosaji 21,836 walilipa faini mbalimbali zaidi ya shilingi milioni 655.
Katika kipindi kama hicho mwaka jana jumla ya wakosaji 21,778 walilipa faini
mbalimbali zaidi ya shilingi milioni 653.3. Faini hizo ni sawa na ongezeko la
asilimia 0.3”, amesema kamanda huyo.
ACP Magiligimba ametaja
baadhi ya mikakati mbalimbali ya kukabiliana/kupunguza zaidi uhalifu, wahalifu
na ajali za barabarani kuwa ni kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani
kupitia vyombo vya habari na kushirikiana na asasi mbalimbali katika kutoa
elimu na matengenezo ya barabara.
“Vile vile tutaendelea
kuimarisha ushirikiano zaidi na asasi zisizo za kiserikali, ikiwemo World
Future Vocation, mabalozi wa usalama barabarani na SUMATRA. Pia tutashirikiana
na TANROADS, Halmashauri za Wilaya na manispaa kushauriana namna ya kufanya
matengenezo ya barabara katika maeneo yaliyoharibiwa au yenye kusababisha ajali
za mara kwa mara”, amesema ACP Magiligimba.
Kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoa wa Singida, ACP,Debora Daud Magiligimba, akitoa taarifa juu ofisini kwake.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments