Breaking News

Mfanya biashara agundulika akiwa amefariki Dunia Mkoani Singida





Mfanya biashara agundulika akiwa amefariki Dunia Mkoani Singida





SINGIDA

Mfanyabiashara Tausi  Hamisi @ Angel Edward, (39), Msubwa  mkazi wa Ipembe – Manispaa ya Singida akutwa akiwa amefariki Dunia pembeni mwa choo cha wanawake cha Hoteli ya KBH iliyopo katika Maeneo ya KBH Hotel, Kata ya Mughanga, Tarafa ya Unyakumi Manispaa ya Singida.



Akiongea na waandishiwa wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Debora D. Magiligimba  jana amaeleza kuwa tukio hili lilitokea siku ya tarehe 24.08.2017 majira ya saa 11:30 alfajiri ambapo ameeleza kuwa  Chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana



Kamanda Magiligimba meeleza kuwa  Jeshi la Polisi limefanya uchunguzi wa awali wa tukio hilo na kubaini kuwa Mareheumu aliondoka nyumbani kwao siku ya tarehe 23.08.2017 jioni na kuambatana na wenzake kwenda katika ukumbi wa UHASIBU ambapo kulikuwa na harusi. Baadae usiku huohuo walikwenda katika ukumbi wa Sky way Night Club kuendelea na starehe.



Hata hivyo Kamanda ameeleza kuwa usiku huo huo  walitoka Sky way Night Club na kwenda Maeneo ya KBH Hotel akiambatana na rafiki yake aitwaye Salima Mohamed, (28), Mkulima na mkazi wa Majengo – Manispaa ya Singida na Mwanaume mwingine ambaye hakufahamika kwa Majina wala makazi ambapo inasemekana waliendelea na starehe Hotelini hapo wakiwa watatu ambapo ilifikia muda Marehemu akaenda kujisaidia ndipo Mwanaume waliyekuwa naye alimfuata na hawakurudi tena hadi mlinzi alipogundua mwili wa Marehemu siku ya tarehe 24.08.2017 majira ya saa 11:00 alfajiri.



Kuhusiana na tukio hilo ACP  Magiligimba ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia Watu wawili ambao ni Haruna Athuman, (34), Mlinzi wa KBH Hoteli mkazi wa Kindai Manispaa ya Singida na Salima Mohamed, (28),  kwa mahojiano.



Kamanda Magiligimba amesema Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa  Singida kwa uchunguzi wa Daktari na baada ya uchunguzi kuakamilika utakabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za mazishi na akatoa wito kwa Wananchi kubadilika na kuacha kuambatana na watu wasiowafahamu katika maeneo ya starehe na pia inapotokea wawe wepesi wa kumdadisi mtu kujua kama ni mtu mwema na wanapomtilia mashaka, watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ili watu hao wakamatwe kabla hawajatekeleza vitendo vya uhalifu.





Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814




1 comment: