Mamlaka za maji na mabonde ya maji zatakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato
Mamlaka za maji na mabonde ya maji kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Picha/habari Na
Nathaniel Limu.
SINGIDA.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amezihimiza mamlaka za maji na mabonde
ya maji kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kujiendesha vyenyewe
bila kutegemea Serikali kuu.
Profesa
Mkumbo ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka ya maji
Singida (SUWASA), Bonde la maji kanda ya kati na maabara, mjini hapa mjini .
Amesema
Serikali haina fedha za kukidhi mahitaji yote ya mamlaka za maji na mabonde Cchini hivyo ni vema vikaweka mikakati ya kujitengemea kimapato.
“Duniani kote
hata Marekani haitoi fedha kwa taasisi kama hizi zenu. Tumieni kalamu na akili
zenu kwa ajili ya kuandika maandiko yatakayowasaidia kupata fedha za
kujiendesha bila kutegemea serikali au wafadhili”, amesisitiza.
Akisisitiza
zaidi, kwa kusema umefika wakati sasa mamlaka na mabonde ya maji, zifikirie
kuwekeza na kujiwekea mipango thabiti ya kuongeza mapato yao.
Aidha, Katibu
Mkuu huyo amewataka watumishi wa SUWASA, kutoa huduma bora itakayovutia
wananchi wengi zaidi kupata huduma ya maji katika mamlaka hiyo.
“Wateja
wa maji ndio wanaowalipa ninyi mishahara na stahiki zingine. SUWASA ikiwa
na wateja wachache kwa vyo vyote uendeshaji wake utakuwa mgumu na hivyo hivyo
upatikanaji wa mishahara yenu nao utakuwa mgumu”, amesema Profesa Mkumbo.
Ameongeza
kuwa SUWASA na mamlaka nyingine za maji Cchini ni lazima ziwe na mkakati wa
kupanua wigo wa wateja.
“Utamaduni wa
kutoa huduma bora unamfurahisha mteja na atapenda kuendelea kuwa mteja wa
SUWASA wakati wote. Pia itawavutia watu wengi kukimbilia huduma bora
zinazotolewa na SUWASA”,alisema.
Katika
hatua nyingine, Profesa Mkumbo ametumia nafasi hiyo kusisitiza utaratibu wa kulipia
kwanza (pree paid) maji kabla ya kupata huduma ya maji.
Amesema
utaratibu huo utasaidia kuepukana na wateja wakorofi ambao huzalisha
madeni sugu na kusababisha mamlaka kushindwa kutoa huduma zinazokidhi mahitaji
ya wateja.
“Kupitia
utaratibu huu mteja husika ni lazima ajue matumizi yake ya maji kwa kipindi cha
mwezi. Baada ya hapo analipia kiwango hicho cha maji halafu ndipo apewe maji ya
kiwango alicholipia”, amesema katibu mkuu huyo.
Awali
Afisa Maji bonde la kati Benard Chikarabhani amesema wameanza utekelezaji wa
ujenzi wa bwawa la Farkwa kwa lengo la kuongeza usambazaji wa maji katika mji
wa Dodoma, Bahi, Chamwino na halmashauri ya wilaya Chemba.
“Bwawa hilo
linatarajiwa kuwa na kiasi cha maji cha mita za ujazo 470,000,000 na litachukua
eneo la kilometa za mraba 68 pia bwawa litatumika kuboresha kilimo cha
umwangiliaji katika mradi wa umwangilaji Bahi”, amesema Chikarabhani.
Wakati
huo huo, Chikarabhani amesema bodi ya maji bonde la kati inatarajia kutumia
zaidi ya shilingi bilioni 2.4 kugharamia ujenzi wa ofisi ya Makao makuu mjini
hapa.
“Fedha hizo
zitagharamia pia ukarabati wa Ofisi na Maabara katika Ofisi ndogo ya bodi
zilizopo Mkoani Shinyanga. Vile vile ujenzi wa ofisi ya jumuiya ya watumijai maji
ya Mto wa Mbu”, amesema afisa huyo
Katika kile kinachoonekana
kutekeleza dhana ya 'hapa kazi tu', Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akipanda juu ya
tanki kuchungulia maji katika vyanzo vya maji kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida.
Katibu Mkuu
Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo
akiambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina M Lutambi(katikati)
na Mhandisi wa maji SUWASA Robert Sunday (kushoto), wakikangua vyanzo vya maji
kijiji cha Mwankoko Mnispaa ya Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya
Maji Profesa Kitila Mkumbo (wa pili kulia) akipewa ufafanuzi wa mashine ya
kupampu maji katika chanzo cha maji cha kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida
na Mhandisi wa SUWASA Patrick Nzamba.
Mhaidrolojia bonde la
maji la kati Robert Sunday akichangia hoja kwenye mkutano ulioitishwa kwa ajili
ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuzungumza na watumishi wa SUWASA,
bonde la maji kati na maabara.
Katibu Mkuu Wizara
ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watumishi watumishi wa Mamlaka
ya SUWASA, bonde la maji la kati na maabara mjini hapa. Wa kwanza kulia ni Mhandisi
SUWASA, Patrick Nzamba.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments