Wanawake Singida wahimizwa kujenga utamaduni wa kujiamini na kuondoa woga
Wanawake Singida wahimizwa kujenga utamaduni wa kujiamini na kuondoa woga
Wanawake Mkaoni
Singida wamehimizwa kujenga utamaduni wa kujiamini na kuondoa woga, ili waweze
kufanikiwa kupigania haki zao za msingi, ikiwemo ya haki ya kumiliki ardhi.
Wito huo umetolewa na
diwani wa kata ya Mungumaji Hassan Shabani Mkata, wakati akichangia mada juu ya
haki ya umiliki wa ardhi kwa wanawake kwenye mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa kituo cha walimu mjini hapa.
Mafunzo juu ya haki ya
mwanamke kumiliki ardhi yaliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Singida
IR Vicoba Net Work (SIRVICONET) na kufadhiliwa na shirika la The Foundation for
Civil Society kwa ajili ya wanawake wa Singida.
Mkata amefafanua kuwa
katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua uhalali wa umiliki ardhi
kwa wanawake, isipokua wanawake wenyewe wanakosa haki hiyo kutokana na woga wao
uliopitiliza.
Amesema umefika
wakati sasa wanawake wawe mstari wa mbele kupingania haki zao na kutokomeza
mila kandamizi, ziliyopitwa na wakati ambazo zinawakandamiza kwamba hawana haki
ya kumiliki ardhi.
“Kwa hilo wanawake watafanikiwa
tu endapo wataondoa woga, wakajiamini na wakaunganisha nguvu zao. Nasisitiza,
wanawake wanapaswa kutambua kuwa wanahaki sawa na wanaume, katika kumiliki
ardhi”, amefafanua.
Naye mwezeshaji wa
mafunzo hayo Afisa Ardhi kutoka Manispaa ya Singida, Lilian Msasi amesema ardhi
ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa rais, kwa niaba ya Watanzania wote.
“Raia wote…. wanawake
na wanaume wana haki sawa ya kupata, kumiliki, kutumia na kugawana ardhi.
Miliki za ardhi zilizopo zinatambuliwa na kulindwa kisheria”, amesema Msasi.
Msasi amesema
mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika kupata, kumiliki, kutumia na kugawa
ardhi. Haki hiyo imetamkwa kwenye kifungu cha tatu (92) cha sheria ya ardhi
mjini na sheria ya vijiji za mwaka 1999.
Kuhusu sifa za kuomba
haki ya kumiliki ardhi, Lilian amesema kuwa ni mtu ye yote mwanamke au
mwanaume, mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anaweza kupatiwa hati
ya kumiliki ardhi.
“Pia kikundi cha watu
ambao sio raia wa Tanzania, wanaweza kuomba haki ya kumiliki ardhi (delivative
righs), kwa ajili ya uwekezaji”, amesema.
Ameongeza kuwa kwa
vile wanawake ni watumiaji wakuu wa ardhi, vyombo vinavyohusika na masuala ya
usimamizi na utendaji wa ardhi, vihakikishwe kuwa wanawake na wanaume
wanashirikishwa ipasavyo katika masuala yahusuyo ardhi
Awali Mratibu wa Shirika
la SIRVICONET, Happy Francis, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo
zaidi wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata, maafisa watendaji wa kata na
maafisa maendeleo ya jamii, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
zaidi.
Ameongeza kuwa dhamira
ya SIRVICONET ni kuwezesha wanachama wake kuwa na nguvu kiuchumi katika
kupambana na umaskini, ujinga na maradhi na kuwa na mahusiano mazuri miongoni
mwao.
Mratibu wa shirika
la Singida IR Vicoba Net work (SIRVICONET) Happy Francis, akitoa ufafanuzi
wa jambo kuhusu mafunzo juu ya umiliki ardhi kwa wanawake. Mafunzo hayo yamefanyikia
kwenye ukumbi wa mikutano kituo cha walimu barabara ya Nyerere mjini hapa.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo juu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake yaliyoandaliwa na
shirika la SIRVICINET na kufadhiliwa na shirika la The Foudation For Civil
Society.
Mwezeshaji
Lilian Msasi, akitoa mafunzo juu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake
yaliyoandaliwa na shirika la SIRVICONET na kufadhiliwa na shirika la The Foundation
For Civil Society.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na
ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments