Breaking News

Watu sita wamefariki Dunia Mkoani Singida na wengine 22 kujeruhiwa baada Gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.



Watu sita wamefariki Dunia Mkoani Singida na wengine 22 kujeruhiwa baada Gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.

 Watu sita wamefariki Dunia Mkoani Singida na wengine 22 kujeruhiwa baada Gari lenye namba za usajili T.806 AEL SCANIA lori mali ya Abdalla Mussa, (39), Mnyaturu, Mfanyabiashara na Mkazi wa Mwenge Singida, likiendeshwa na Dereva aliyekimbia baada ya ajali hiyo anayefahamika kwa jina la  Juma Jumanne @ Kidanka, (32),  Mnyaturu,  na mkazi wa Mnung’una-Singida likitokea Mtinko kwenda Singida kupinduka.  

Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kweke hii leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora D. Magiligimba ameeleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1:30 usiku huko katika Kijiji na Kata ya Kijota, Tarafa  ya Mtinko, Wilaya Singida  barabara ya  Mtinko – Ilongero,



Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa  ni pamoja na Haji Jumanne, Mnyaturu, umri kati ya miaka 28-35, mkazi wa Mrama, Mikidadi  Mohamed, Mnyaturu, umri kati ya miaka 35-40, Mkazi wa Ilongero na Musa  salim, Mnyaturu, umri kati ya miaka 35-40, mkazi wa Mwakiti.



Wengine ni Allen Mwangu,  Mnyaturu, umri kati ya miaka 30-38, mkazi wa Ikungi, Lucas  Stephano, mnyaturu, miaka 40, mkazi wa mlama na Sharifa  Omari, mnyaturu, miaka 19, mkazi wa Ilongero wilaya ya Singida vijijini.



Aidha Kamanda amewataja waliojeruhiwa kuwa  ni pamoja na Fadhili Jumanne , (33),  Mnyaturu, Mkazi wa Kibaoni - Singida, Mikidad Hamisi, Jafari Hamis, na Idrisa Ibrahimu, ambao wote wamevunjika miguu na kulazwa katika Hospitali ya Hydom, Mkoani Manyara na hali zao siyo nzuri.

Wengine ni Samwaga Hango, (26) Mnyaturu, Mkazi wa Singida Mjini, amevunjika mguu wa kushoto, Hamza Hassani, (24), Mnyaturu, Mkazi wa Singida Mjini amevunjika mguu, Mwajuma Rajabu , (45) Mnyaturu, Mkazi wa Ilongero amepasuka bandama pamoja na majeruhi wengine 10 wamepata maumivu sehemu mbalimbali za miili yao na  wamelazwa katika Hospitali ya Misheni Mtinko.



Majeruhi wengine ni Asha ramadhani, (42), Mnyaturu, Francisca John, (43), Muhango, Mariamu Juma, (50), Mhango wote wakazi wa Irongero ambao wamelazwa katika Hospitali ya Ilongero na Nuru said (19), Mnyaturu, Mkazi wa Ilongero, amevunjika paja la kushoto na maumivu Mkono wa kulia,  Ally Ibrahim, (21), mnyaturu,Mkazi wa Ilongero ambao amevunjika mguu wa kulia na wote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida na hali zao siyo nzuri.



Ametaja Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa Dereva kutokuwa makini akiwa anaendesha gari hilo barabarani pamoja na kupakia mzigo kwa njia ya hatari.



Hata hivyo uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa kabla ya ajali hiyo siku ya tarehe 12.08.2017 Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Singida SP Peter Majira alifanya kikao na wamiliki wa magari ya mizigo akiwepo Mmiliki wa Gari iliyopata ajali ambapo alitoa elimu juu ya matumizi sahihi ya magari ya mizigo. Hata hivyo pamoja na elimu hiyo kutolewa, Mmiliki wa gari Abdala Mussa alikaidi maelekezo hayo na kupelekea ajali hiyo kutokea.



Kuhusiana na ajali hiyo, Jeshi la Polisi linamshikilia Mmiliki wa Gari kwa mahajiano na baada ya mahojiano kukamilika atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake na Juhudi za kumtafuta dereva aliyesababisha ajali hiyo zinaendelea.



   ACP Magiligimba hakusita kutoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya moto kusimamia vema matumizi sahihi ya magari yao kulingana na sheria na taratibu za usalama barabarani na kuongeza kuwa Endapo gari imesajiliwa kwa matumizi ya kubeba mizigo, itumike kwa kubeba mizigo na siyo kuchanganya mizigo na Abiria na kama gari imesajiriwa kwa matumizi ya kubeba abiria, itumike kubeba abiria siyo kuchanganya Abiria na mizigo.

Kamanda Magiligimba hakuacha kutoa wito kwa a wito kwa wananchi/abiria kwa kuwaasa kuacha tabia ya kupanda katika magari ya mizigo kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani 

Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814

 



1 comment: