Breaking News

Idadi ya Watahiniwa wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi Mkoa wa Singida yaongezeka kwa asilimia 35%


Idadi ya Watahiniwa wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi Mkoa wa Singida yaongezeka kwa asilimia 35%


Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814


Na. Sylvestare Richard

SINGIDA.
Idadi ya Watahiniwa wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi Mkoa wa Singida inayoanza leo imeongezeka hadi kufikia wanafunzi 28,947 kutoka wanafunzi 21, 417 waliofanya mitihani hiyo hiyo mwaka jana.

Ongezeko hilo la wanafunzi 7,530 ni kiashiria cha kuboreshwa kwa elimu na usimamizi wa sekta ya elimu msingi kwa Mkoa wa Singida pamoja na jitihada za wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria masomo yao ipasavyo.

Hayo yamebainishwa jana na Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian Kimolo ambaye amefafanua kuwa jumla ya wasichana 15,964 na wavulana 12,984  wameungana na wenzao Nchi nzima kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya darasa la saba hapo jana kwa kuanza kufanya mtihani wa Kiingereza ukifuatiwa na mtihani wa Hisabati.

Kimolo ameeleza kuwa ongezo la wanafunzi wanaofanya mitihani inaweza kusababishwa na idadi kubwa ya udahili wa wanafunzi hao kwa mwaka walioanza darasa la kwanza, lakini pia sababu nyingine kubwa ni usimamizi mzuri katika sekta hiyo ambao umepunguza utoro wa wanafunzi uliokuwa ukipelekea wanafunzi hao kuacha shule.

Amefafanua kuwa wanafunzi wanaweza kudahiliwa wengi lakini wakamaliza wachache kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, kuacha shule, uhamisho, na vifo hivyo idadi ya watahiniwa inapoongezeka  ni ishara kuwa walimu, wazazi/walezi na idara za elimu ngazi zote zimefanya kazi nzuri ya kusimamia sekta hiyo.

Kimolo amesema mitihani imeanza kufanyika kwa amani na utulivu kutokana na kuwa ofisi yake imefanya maadalizi mapema kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na halmashauri zote za Mkoa wa Singida.

Aidha amewataka wasimamizi kuzingatia maadili, kanuni na sheria walizoelekezwa wakati wa semina za usimamizi ili mitihani ifanyike kwa haki bila ya matatizo yoyote.

Kimolo ameongeza kuwa jumla ya vituo vya kufanyia mitihani hiyo kwa mkoa wa Singida ni 518 huku mikondo ikiwa 1313 huku akiwasisitiza wanafunzi hao kufanya mitihani kwa amani na nidhamu.

Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814



No comments