Kanisa Katoliki Jimbo la Singida lapongezwa kwa uamuzi wake wa kuwaelimisha vijana 490 umuhimu wa kulipa kodi.
Kanisa Katoliki Jimbo la Singida lapongezwa kwa uamuzi wake wa kuwaelimisha vijana 490
umuhimu wa kulipa kodi.
Habari/Picha na Nathaniel
Limu.
SINGIDA.
Mbuge Viti Maalum
(CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, amelipongeza kanisa la Romani
Katoliki (RC) jimbo la Singida kwa uamuzi wake wa kuwaelimisha vijana 490
umuhimu wa kulipa kodi.
Mattembe ametoa
pongezi hizo wakati akizungumza kwenye kongamano la vijana waumini wa kanisa
hilo lililofanyika kwenye jukwaa la askofu Mabula kwenye viwanja vya kanisa
katoliki mjini hapa.
Amesema vijana
wakiwezeshwa kutambua mapema umuhimu wa kulipa kodi na manufaa yake, nchi
itakuwa ya walipa kodi ambao watalipa kwa hiyari yao bila kushurutishwa.
“Suala la kulipa kodi
ni muhimu mno kwa maendeleo ya nchi yoyote hapa duniani. Rais wetu Dkt
Magufuli ameleta mageuzi makubwa mno yanayohusu kulipa kodi. Anajua umuhimu wa
kulipa kodi kwa sababu bila kodi hakuna maendeleo. Baba Askofu, kitendo chenu
cha kutoa elimu ya kodi kwa vijana hawa mtakuwa mmemuunga mkono rais Magufuli
na hongereni sana”, amesema Mattembe.
Mbunge huyo amewataka
vijana hao ambao wametoka wilaya zote za mkoa wa Singida,wakawe mabalozi wazuri
katika kueneza elimu ya kulipa kodi kwa wenzao ambao hawakubahatika kuhudhuria
kongamano hilo.
“Vijana wenzangu
haya maendeleo makubwa mnayoyaona ya barabara nzuri, vituo vya afya na visima
vya maji na maengine mengi, yote yanagharamiwa na fedha za kodi na si
vinginevyo. Serikali ya awamu ya tano inamtaka kila mtanzania mwenye sifa ya
kulipa kodi alipe, tena kwa wakati bila ya kushurutishwa”, amesisitiza.
Aidha amaewataka vijana
wote mkoani hapa wenye sifa ya kufanya kazi, wajiunge kwenye vikundi vya
ujasiariamali pamoja na vile vya kilimo cha biashara, ili waweze kujiletea
maendeleo na kujikomboa kiuchumi.
“Faida za kujinga
kwenye vikundi vilivyosajiliwa ni nyingi ikiwemo ya kupata mikopo kwa masharti
nafuu kutoka taasisi za kifedha. Tunayo maeneo ya kutosha kwa ajili ya ufugaji
nyuki. Mazao ya nyuki yana soko kubwa ndani na nje ya nchi. Anzisheni vikundi
vya ufugaji nyuki mtaharakisha kujikomboa kiuchumi. Nina uhakika serikali ya
mkoa na ofisi yangu tutawasaidia ili muweze kufikia malengo yenu”, amesema.
Mattembe ameahidi
kuchangia mizinga ya kisasa ya kutosha kwa vijana watakaojiunga katika vikundi
huku akiungwa mkono na Katibu wa Jumuiya ya Wanawake (CCM) Manispaa ya Singida
Magreth Malecela ambaye ameahidi kuchangia mizinga mitano ya kisasa.
Awali Baba askofu wa
jimbo la Singida Edward Mapunda amesema vijana hao pia wamepewa elimu juu ya
ujasiriamali, kilimo cha biashara na maadili mema.
Aidha, amesema
kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka mara moja, linatarajia kupanua
wigo kwa kupata wawezeshaji wa fani mbalimbai kutoka nje ya mkoa.
Mbunge wa Viti Maalum
(CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe na Askofu Kanisa Katoliki Jimbo la
Singida, Edward Mapunda wakipongezana kwa kazi nzuri ya kuwaelimisha vijana katika
kongamano la vijana wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida.
Baadhi ya vijana
Kanisa Katoliki Jimbo la Singida waliohudhuria kongamano la wiki moja, lililofanyika
kwenye jukwaa la Askofu Mabula mjini Singida.
Mbunge wa Viti Maalum
(CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe akitoa nasaha zake kwenye kongamano la
vijana wa kanisa katoliki jimbo la Singida.
Baba Askofu Kanisa
Katoliki Jimbo la Singida, Edward Mapunda akizungumza kwenye kongamano la juma
la vijana kanisa katoliki. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida
Aysharose Mattembe.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na
ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments