NMB yatakiwa kuwasaidia wafanyabiashara Mkoani Singida.
SINGIDA.
Benki ya NMB
imetakiwa kuwasaidia wafanyabiashara Mkoani Singida kuanzisha kiwanda cha
kutengenea vifungashio, ili waweze kuhifadhi bidhaa zao katika ubora unaokubalika
kitaifa na kimataifa.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo hapo jana wakati akifungua warsha
ya siku moja ya klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB, katika ukumbi wa Kanisa
Katoliki mjini Singida.
Dkt Nchimbi amesema
klabu hiyo ya wafanyabiashara itaweka alama kubwa katika maendeleo endapo
watajipanga na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifungashio hivyo kuliko
kuendelea kuvifuata nje ya Singida au nje ya nchi.
“Uzoefu usipotumika
vizuri unaweza ukawa kikwazo cha kuendelea, msizoee kufuata vifungashio na
label nje ya Singida wakati fursa ipo ya kuanzisha kiwanda hicho Singida”, amesema
na kuongeza kuwa,
“Wafayabiashara
mzipende biashara zenu na kuziweka katika hali ya usafi na yenye kuvutia, wengine
wanapenda kujisafisha na kujipendezesha wenyewe lakini ukiangalia biashara zao
hazivutii, zimewekwa tu bila kufungashwa vizuri”, amesisitiza.
Aidha amewataka
wafanyabiashara wasiogope kukopa kwakuwa sio jambo la aibu wala fedheha, ila
kinachotakiwa ni kuwa na nidhamu ya mkopo na malengo ili waweze kufanikiwa.
“Akina mama jifunzeni
kuwa na nidhamu ya mkopo, sio unakopa leo mara unasikia kapu la mama, jifikirie
hayo ndio malengo ya huo mkopo hata kama ni jambo muhimu?, nidhamu ya mkopo
inatakiwa ianze kabla ya kukopa na iendelee kuwepo.
Dkt Nchimbi pia
ameishukuru benki hiyo kwa kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali ya
kielimu na afya, pia amewashukuru kwa kutoa mikopo kwa watumishi wa umma jambo
ambalo linawasiadia katika mambo mbalimbali.
Naye Meneja wa NMB
Kanda ya kati Straton Chilongola amesema klabu za wafanyabiashara nchini ziko
34 ambazo zimekuwa zikipatiwa mafunzo mikopo kutoka katika benki hiyo.
Chilongoloa amesema
benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo juu ya ulipaji kodi, ujasiriamali, masuala ya
mitaji, leseni na ardhi ili wafanyabiashara hao waweze kukuza mitaji yao.
Amesema benki hiyo
imefanikiwa kuwakuza wafanyabiashara wengi ambazo wameanza nao wakiwa
wafanyabiashara wadogo ambapo sasa wamekuwa wakubwa na wakati huku wakiajiri
wengine na hivyo kukuza uchumi.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB Singida Emmanuel Rweyemamu
Kyoma amesema wazo la kuanzisha kiwanda cha kutengeza vifungashio wamelipokea
vizuri huku wakijipanga kuandaa andiko kwa ajili ya kiwanda hicho.
Kyoma amesema kwa
ushirikiano na NMB kiwanda hichokitaweza kujengwa Singida huku wakimuahidi Mkuu
wa Mkoa kuwa Mkoa wa Singida utazalisha chakula cha kutosha kulisha Mkoa wa
Dodoma.
Amesema benki ya NMB
imekuwa ikishirikiana na wafanyabiashara hao hivyo mipango ya kukuza uchumi
kama huo wa kuanzisha viwanda utatekelezeka bila matatizo yoyote.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu ya
wafanyabiashara wateja wa NMB Singida Emmanuel Rweyemamu Kyoma mapema leo kabla
ya kufungua warsha ya siku moja ya klabu hiyo, katika ukumbi wa Kanisa Katoliki
mjini Singida.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua baadhi ya bidhaa za wafanyabiashara wateja
wa NMB Singida mapema leo kabla ya kufungua warsha ya siku moja, katika ukumbi
wa Kanisa Katoliki mjini Singida.
Meneja wa NMB Kanda
ya kati Straton Chilongola akizungumza klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB
Singida mapema leo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja, katika ukumbi wa
Kanisa Katoliki mjini Singida.
Wafanyabiashara wateja
wa NMB Singida wakiwa katika warsha ya siku moja katika ukumbi wa Kanisa
Katoliki mjini Singida mapema leo.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments