Waagizwa kuhakikisha hakuna vifo wala majeruhi....................................................................
Wamiliki wote wa
migodi wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini Mkoani Singida wameagizwa kuhakikisha
kuwa hakuna vifo wa majeruhi katika maeneo yao kutokana na uwepo wa miundombinu
mibovu au uzembe wowote.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo alipotembelea mgodi wa madini katika
Kijiji cha Konkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, Wilaya ya Iramba kuona
shughuli za uokoaji mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa
kufariki.
Dkt Nchimbi amesema
wamiliki wa migodi wanatakiwa kuwekeza katika kuboreha miundombinu ya migodi ili
wachimbaji waweze kufanya kazi katika mazingira ambayo si hatarishi.
“Madini yanatakiwa
kuleta neema na kukuza uchumi wa Taifa letu na sio kuangamiza nguvu kazi na
kuleta majonzi, Serikali haiwezi kukubali kupoteza vijana kutokana na uzembe wa
baadhi ya watu”, amesema.
Ameongeza kwa kumtaka
Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kati Sostenes Masolla kuweka ratiba ya
kutoa mafunzo kila wiki huku akitakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili
wachimbaji wapewe semina na mafunzo ya juu ya usalama wao wawapo migodini.
Dkt. Nchimbi pia
amemtaka Kamishna huyo wa madini kufuatilia taaluma na sifa zinazotumika
kuchagua wakaguzi wa migodi maarufu kama ‘inspekta’ kwakuwa wao ndio hutakiwa
kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kuwa shimo au duara liko salama kabla ya
kuruhusu uchimbaji kufanyika.
“Hawa ma inspekta
hawa wasituulie vijana kutokana na uzembe wao, unakuta hajakagua vizuri halafu
anaruhusu watu walipue baruti matokeo yake ndio kama haya, hawa wakiwa makini
ajali za kwenye migodi zitapungua sana”, amesisitiza.
Aidha Dkt Nchimbi
amewataka wachimbaji na wamiliki wa migodi kuachana na imani potofu kuwa endapo
vifo vinatokea katika shimo la mgodi hapo panakuwa na madini mengi.
Amesema ikiwa
atabaini kuwa imani hizo zinaendekezwa na kipa endapo patatokea tena kifo
katika mgodi huo basi hatasita kufunga shughuli za uchimbaji katika mgodi huo.
Kwa upande wao
wachimbaji wameeleza kuwa ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa mgakuzi wa
shimo hilo ambaye aliruhusu ulipuaji wa baruti wakati mazingira yakiwa
hayaruhusu.
Wachimbaji hao
wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa wamekosa amani kutokana na vifo hivyo ambavyo kwa
kiwango kikubwa vimetokana na uzembe huku pia wakilalamikia utaratibu wa malipo
yao.
Mmoja wa wachimbaji
hao Abuu Amiri amesema ma inspekta hao wamekuwa wakijali maslahi binafsi badala
ya kuangalia usalama wa wachimbaji watakaoingia katika shimo hilo.
Mgodi ujulikanao kwa
jina la Sekenke 1 katika kitalu namba 1, ambapo maduara matano
yanayomilikiwa na Marijan Ramadhani na Jakobo Ntobi, yalititia mnamo tarehe
tisa Septemba na kusababisha vifo kwa wachimbaji wawili huku mmoja tayari mwili
wake ukiwa umepatikana na majeruhi watano.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wachimbaji alipotembelea mgodi wa
madini katika Kijiji cha Konkilangi, Wilayani Iramba kuona shughuli za uokoaji
mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki. Kushoto
kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula.
2. Wachimbaji wakiendelea
na shughuli za uokoaji katika Kijiji cha Konkilangi, Wilayani Iramba mara baada
ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
3. Wachimbaji wakiwa
wanatazama shughuli za uokoaji zikiendelea katika Kijiji cha Konkilangi, Wilayani
Iramba mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
4. Mmoja wa wachimbaji Abuu
Amiri akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowatembelea
kuona shughuli za uokoaji katika mgodi wa madini wa Kijiji cha Konkilangi, Wilayani
Iramba mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
5. Umati wa Wachimbaji uliojitokeza
kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowatembelea kuona
shughuli za uokoaji katika mgodi wa madini wa Kijiji cha Konkilangi, Wilayani
Iramba mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na
ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments