ABAKA WATOTO 14 SINGIDA ASHIKILIWA NA POLISI
SSP ISAYA K. MBUGHI AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE. |
ABAKA WATOTO
14 SINGIDA ASHIKILIWA NA POLISI.
Na Sylvester Richard.
SINGIDA.
Mtu mmoja
nayejulikana kwa jina la Daudi Idd @
Karatu Babu, (74), Mganga wa kienyeji anayeishi
katika Mtaa wa Unyankindi katika Manispaa ya Singida anashikiliwa naJeshi la Polisi
Mkoani humo kwa kosa la kubaka watoto wapatao 14.
Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake hii leo
majira ya 4:30 asubuhi Kaimu Kamanda wa Polisi Singida SSP Isaya K. Mbughi
ameeleza kuwa Mtuhumiwa aligundulika kutenda kosa hilo siku ya tarehe
16.10.2017 majira ya 11.45 jioni huko Maeneo ya Unyankindi, Mtaa wa Minga Kata ya
Mitunduruni, Tarafa ya Mungumaji Manispaa ya Singida ambapo Mtoto mwenye umri
wa miaka 7, jina lake linahifadhiwa , Mwanafunzi wa Darasa la II katika Shule
ya Msingi Unyankindi akiwa anaogeshwa na Mama yake alidai kuwa anahisi maumivu
makali sehemu zake za siri na Mama huyo alipomdadisi Mtoto alisema kuwa
alibakwa na Mtu aitwaye Daudi Idd @
Karatu Babu, Mganga wa kienyeji anaishi karibu na Shule ya
Msingi Unyankindi.
Kaimu Kamanda Mbughi ameeleza kuwa baada ya Mama huyo
kubaini maumivu ya mwanae alimchunguza Mtoto wake na kugundua kuwa anamichubuko
sehemu za siri ndipo alipoenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Minga
ambapo kwa kushirikiana na Polisi Kata ya Minga walikwenda moja kwa moja nyumbani
kwa mtuhumiwa Daudi Idd @ Karatu Babu
ambapo walipofika walikutana na watoto wengine wakitoka nyumbani kwa Mtuhumiwa ambao
nao baada ya kuhojiwa walidai kuwa nao wamebakwa.
Mbughi amesema kuwa kuhusiana na tukio hilo watuhumiwa
wawili ambao ni mtuhumiwa Daudi Idd @ Karatu Babu na Mwanae wa kumlea Abdallah Yahaya
@ Kola, (31), Dereva wanaoishi katika nyumba moja na Jeshi la Polisi na
kutanabaisha kuwa uchunguzi wa awali umefanyika na kubaini kuwa mtuhumiwa Daudi Iddi amekuwa akiwabaka
watoto wenye umri kati ya maiaka 7 na
12 kwa nyakati tofauti tangu Desembe
2016 hadi Octoba 2017 ambapo Mpaka
kufikia siku ya tarehe 16.10.2017 watoto wapatao 14 majina yanahifadhiwa
ambao ni wanafunzi wa Shule za Msingi
tofauti zikiwemo shule za Unyankindi,
Singidani, Shule ya Nyerere na Shule ya Msingi Muhanga wamelalamika kubakwa na
mtuhumiwa huyo.
SSP Mbughi amesama kuwa mbinu aliyokuwa akiitumia mtuhumiwa
kufanikisha ubakaji huo kuwa ni kuwarubuni watoto wa kike kwa kuwaonyesha video
/movie kwenye kompyuta mpakato (raptop) na wakati huo akiwa mmoja mmoja kwa
nyakati tofauti anatumia muda huo kuwaingilia kimwili au kuwachezea sehemu zao
za siri ambapo watoto hao walizoea kila unapofika muda wa mapumziko na muda wa
mchana baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani watoto hao hupita nyumbani kwa
watuhumiwa kwa lengo la kuangalia video na ndipo hbakwa na baada ya kuingiliwa watoto hao hupewa kati ya Tsh.
200/= hadi Tsh. 2,000/= na pipi kama zawadi yao
na kuwapaka unga kwenye paji la uso na kuwatishia kuwa kama wangemwambia
mtu wangekufa kwa kuwa yeye ni Mganga wa tiba asila. Hata hivyo ulifanyika
upekuzi ndani ya nyumba hiyo wanayoishi watuhumiwa na kufanikiwa kupata pipi
ambazo watuhumiwa huzitumi kuwarubuni watoto.
Mbughi ameeleza kuwa Jeshi la Polisi lilifika katika
Shule husika na kufanikiwa kuwapata wototo 14 wanaosadikiwa kubakwa na
watuhumiwa na Kwa kushirikiana na Daktari, watoto walifanyiwa vipimo katika
Hospitali ya Mkoa Singida na kubainika kuwa watoto 12 wameingiliwa kimwili na
kuongeza kwa kusema kuwa watuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano
zaidi na baada ya mahojiano kukamilika watafikishwa mahakani kwa makosa ya
Kubaka, Shambulio la aibu na Kula njama kutenda kosa.
Kaimu Kamanda Mbughi ametoa rai kwa wazazi kuwa makini
na mienendo ya watoto wao na kuwa nao karibu ili kujua mienendo yao hali ambayo
itasaidia kuzuia vitendo vya kikatili kwa watoto.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments