(SACP) FORTUNATUS AWATAKA MADEREVA WOTE TANZANIA KUENDESHA VYOMBO VYAO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
(SACP) FORTUNATUS AWATAKA MADEREVA WOTE TANZANIA KUENDESHA VYOMBO VYAO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu amewataka Madereva wote
Tanzania kuendesha vyombo vyao kwa
kuzingatia sheria kanuni na taratibu
za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima hasa katika
kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya kwa lengo la
kumaliza mwaka huu na kuanza mwaka ujao 2018 salama.
Akiongea na Madereva pamoja na wananchi waliojitokeza kumsikiliza
katika eneo la Stendi ya Daladala iliyopo karibu na Stendi ya zamani ya Mabasi
katika Manispaa ya Singida amewataka madereva kutokuidhalilisha kazi yao kwa
kushindwa kufauta sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali ambazo
zinaweza kupelekea majeruhi na wakati mwingena vifo kwa madereva wenyewe,
abiria na watumiaji wengine wa barabara na kuwataka kuheshimu kazi yao kwani
ndiyo kazi waliyoichagua. Amewataka Madereva ambao hawawezi kuzitii sheria hizo
basi bora waiache kazi hiyo la sivyo sheria itachukua mkondo wake dhidi
yao.
Kamanada huyo amechukua nafasi kuwaomba Madereva na wananchi wote
kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu wa aina yeyote
ili wahalifu hao washughulikiwe kisheria na kuongeza kuwa Serikali inahamasisha uwekezaji katika
viwanda kwahiyo amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida na Tanzania yote kwa
ujumla kuimarisha usalama barabarani ili kuiunga mkono Serikali kwani wawekezaji
wanahitaji kuwekeza katika maeneo salama.
Aidha katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi Mkoani Singida
akihamasisha suala zima la usalama Barabarani, Kamanada Muslimu ameweza kukagua baadhi
ya Mabasi yanayofanya safari mbalimbali kupitia Mkoa wa Singida na kubaini kuwa kwa sasa
madereva wengi wa mabasi ya abiria wamekuwa wakitii sheria za usalama
barabarani kwani katika baadhi ya Mabasi aliyoyakagua katika eneo la Mizani Manispaa ya Singida ambapo ukaguzi huo umeenda sambamba na upimaji wa
ulevi kwa Madereva, hakuna Dereva aliyebanika kutumia kilevi cha aina yoyote
huku magari hayo yakiwa na hali nzuri na hakuna basi lililozidisha abiria.
Kamanda amewashukuru baadhi ya Madereva wanaotii sheria na
kuwataka madereva wengine kuiga mfano huo mzuri kwa lengo la kuokoa maisha ya
watanzania wengi wanaopoteza maisha kutokana na ajali.
Nao baadhi ya Abiria wa Mabasi yaliyokaguliwa wamekiri kuona Madereva
wakiendesha kwa kuzingatia Sheria za usalama barabarani na kulishukuru Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani kuendelea kuvisimamia
vyema vyombo vya usafiri na kuwaomba waongeze juhudi ili kupunguza zaidi ajali za barabarani na ikiwezekana kuzimalizia kabisa.
Ikumbukwe kuwa Jeshi la Polisi Mkoani
Singida, limefanikiwa kupunguza ajali za barabarani kutoka ajali 69 kwa kipindi
cha mwaka 2016 hadi kufikia ajali 24 katika kipindi cha mwezi Januari mpaka
Juni mwaka huu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora D. Magilingimba hapo Mwezi Augost 2017.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu Akiongea na Madereva pamoja na wananchi waliojitokeza kumsikiliza
katika eneo la Stendi ya Daladala iliyopo karibu na Stendi ya zamani ya Mabasi
katika Manispaa ya Singida.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu akiwa na askari wengine wa usalama barabarani wakikagua moja ya basi la abiria katika Maeneo ya Mizani Manispaa ya Singida.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu akiongea na abiria katika moja ya basi baada ya kufanya ukaguzi ambapo abiria wameeleza kufurahishwa na utendaji mzuri wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani katika kusimamia vyombo vya usafiri.
Baadhi ya abiria wa moja ya Basi lililokaguliwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu katika Maeneo ya Mizani Manispaa ya Singida.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu akionesha kipima ulevi kwa abiria katika moja ya basi baada ya
Dereva wa Basi hilo kupimwa kilevi na kubaini kuwa hana kailevi cha aina
yoyote.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu akiendelea na ukaguzi wa mabasi ya abairia katika eneo la Mizani Manispaa ya Singida.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu akitoka kufanya ukaguzi katika moja ya basi la abaria huku
akiwa mwenye furaha baada ya kubaini kuwa katika mabasi yote aliyokagua ,
hakuna dereva aliyebainika kutumia kilevi wala kuzidisha abiria katika
mabasi yao.
Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814
No comments