ABIRIA WATAKIKIWA KUTOA TAARIFA ZA MADEREVA WANAOKIUKA SHERIA ZA USLAMA BARABARANI
Kamanda wa
kikosi cha usalama barabarani Tanzania Kamishina msaidizi mwandamizi (SACP) Fortunatus
Musilimu Amewataka abiria wote Nchini kulisaidia Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama
barabara kwa kutoa taarifa za madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani
katika mabasi wanayosafiria ili wakamatwe na sheria kuchukua mkondo wake.
SACP
Musilimu ameeleza hayo wakati akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada
ya kufanya ukaguzi kwa baadhi ya Mabasi yaendayo Mikoani kupitia Mkoa wa Singida
ambapo katika ukaguzi huo ameshirikiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida
ACP Debora D. Magiligimba, RTO Singida SSP Peter Majira pamoja na Kikosi cha
Mbwa kutoka Mkoa wa Singida ambapo mabasi
ya abiria yaliyokaguliwa hakuna basi lililobainika kujaza abaria zaidi ya uwezo
wake na hakuna abiria aliyebainika kubeba madawa ya kulevya kwa mujibu wa
ukaguzi wa mbwa ambao umefanywa na Mbwa wataalamu wa kubaini madawa ya kulevya.
Katika
kuelekea sikukuu za Krimasi na Mwaka mpya ambazo pia zitafuatiwa na kipindi cha
wananchi wengi kusafiri kurudi katika maeneo ya kazi na wanafunzi kurudi Mashuleni
baada ya likizo zao kuisha, Kamanda Musilimu amewataka madereva kuzingatia
sheria za usalama barabarani hasa akiwataka kuacha kuendesha magari kwa mwendo
kasi bila kuchukua tahadhali, kutokuzidisha abiria katika vyombo vyao na kuacha
kuendesha vyombo vyao wakiwa wamelewa na Kueleza kuwa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana
na vikosi vingine limejipanga vizuri kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote ili
wananchi washerehekee sikukuu kwa amani.
Kamanda pia
amewataka wamiliki wa Vyombo vya usafiri kuwasimamia vizuri waajiriwa wao na
kutopandisha nauli kiholela na kutoa onyo kuwa yeyote atakayepandisha nauli
bila uataratibu atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo
Kamanda Musilimu amewaomba Wazazi
kuhakikisha wanakuwa na watoto wao muda
wote ili kulinda usalama wao hasa katika
kipindi hiki cha sikukuu kuliko kuwaacha
wakizagaa barabarani hivyo kuitii kauli mbiu isemayo ‘’Zuia ajali Tii Sheria Okoa maisha’’
Aidha
Kamanda Musilimu amefika Mkoani Singida akiendelea na doria ya Usalama barabarani
ambapo pia amefanya doria katika Mikoa ya Kigoma na Tabora na kwa niaba ya Jeshi la Polisi Tanzania amechukua nafasi hiyo kuwatakia Watanzania wote Heri ya Krismasi na Mwaka mpya 2018.
Naye RPC
Mkoa wa Singida ACP Debora D. Magiligimba amewahidi wananchi wa Mkoa wa Singida
kuwa watasherehekea sikukuu za krismasi kwa amani kwani Jeshi la Polisi Mkoa
limejipanga vizuri kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote kwa kufanya doria
mbali mbali zikiwemo za miguu, doria za magari na doria za mbwa.
Magiligimba
amewataka wamiliki wa Kumbi za starehe kutokujaza watu zaidi ya uwezo wa kumbi
zao na kuchukua nafasi hiyo kuwashukuru
Wananchi wa Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa
ushirikiano mkubwa kwa kutoataarifa za uhalifu na wahalifu na kuwaomba waendelee
kufanya hivyo na kuienzi kauli mbiu isemayo ‘’Tukishirikiana kwa pamoja
Singida bila uhalifu inawezekana''
Katikati aliyeshikilia fimbo ni Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu akiwa na Askari wa kikosi cha Mbwa Singida akikagu basi ili kubaini uhalifu mbalimbali unaoweza kufanyika katika vyombo vya usafiri.
Kamanda wa
kikosi cha usalama barabarani Tanzania Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu akitoa elimu juu ya usalama barabarani kwa abiria katika moja ya basi lililofanyiwa ukaguzi katika maeneo ya Njuki Manispaa ya Singida.
Kulia ni Kamanda wa
kikosi cha usalama barabarani Tanzania Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada kukagua baadhi ya mabasi yanayofanya safari za Mikoani kupitia Singida ambapo aliyesimama katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora D. Magiligimba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora D. Magiligimba katikati akitoa neno kwa waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukagua baadhi ya Mabasi yanayofanya safari za Mikoani kupitia Mkoa wa Singida.
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Namba yetu ya WhatsApp 0629 655814
Facebook - machibya richard.
No comments