DEREVA NA UTINGO WAKE WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LAO KUPINDUKA NA KUUNGUA MOTO KATIKA ENEO LA MLIMA SEKENKE SINGIDA.
DEREVA
NA UTINGO WAKE WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LAO KUPINDUKA NA KUUNGUA MOTO
KATIKA ENEO LA MLIMA SEKENKE SINGIDA.
Na
Syliveater Richard.
SINGIDA.
Watu wawili
wanaume mmoja akisadikiwa kuwa ni Dereva na Mwingine Utingo wamefariki Dunia
Mkoani Singida kutokana na kuungua kwa moto baada ya Gari walikuwa wakisafiria
kupata ajali katika eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
Akiongia na
waandishi wa Habari hii leo Majira ya saa 8:30 mchana katika eneo la Mzani
Singida akiwa katika mwendelezo wa kufuatili taarifa za ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora
D. Magiligimba ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 4:30 asubuhi ambapo Gari Namba
T.167 BQT aina ya Flight Liner Tenker lenye tela Namba T.967 ALX Mali ya
Kampuni ya Petrol mark African yenye Makao yake makuu Jijini Dar es salaam likitokea Dar es salaam –
Mutukula kwa kutumia barabara kuu ya Singida
– Nzega liliacha njia, Kupinduka, Kuungua moto, na kusababisha vifo vya watu
hao.
Ameeleza kuwa
Jeshi la Polisi limefanya uchunguzi wa awali
na kubaini kuwa gari hilo lilipima katika Mzani wa Singida hii leo
majira ya saa 1:27 asubuhi likiendeshwa na Dereva aitwaye Erasto Abed Lusazi
akiwa na Utingo aitwaye Ramadhani Hashimu Ramadhani Wote wakazi wa Tabata Dar
es salaam na ndiyo wanaosadikiwa kufariki katika ajali hiyo.
Mgililigimba
sema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani Singida linaendelea na uchunguzi kuhusiana na
ajali hiyo ili kujua chanzo halisi na kisha kutoa wito kwa madereva wote
kuendelea kutii sheria za usalama barabarani
wa Singida. Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospita ya Wilaya ya
Iramba kwa Uchunguzi wa Daktari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora
D. Magiligimba akikagua eneo la ajali iliyotokea hii leo kaika eneo la Mlima Sekenke Mkoani Singida
Baadhi ya nyaraka zinoonesha jina la mmoja wa watu wawili waliofarika katika ajali iliyotokea hii leo katiia eneo la mlima Sekenke Mkoani Singida
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora
D. Magiligimba akiendelea kufuatilia taarifa za watu waliofariki Dunia kwenya ajali iliyotokea hii leo katika eneo la mlima Sekenke Mkoani Singida. Ufuatiliaji huo umefanyika katika Ofisi za Mzani Singida.
Pichani ni gari lililopinduika likiendelea kuwaka moto hii leo katiia eneo la mlima Sekenke Mkoani Singida.
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Namba yetu ya WhatsApp 0629 655814
Facebook - machibya richard.
No comments