FUVU LA FUVU LA KICHWA CHA MWANAMKE ALIYEPOTEA MIAKA 8 LAPATIKANA KWENYE PANGO LA MBUYU
FUVU LA KICHWA CHA MWANAMKE ALIYEPOTEA MIAKA 8 LAPATIKANA KWENYE PANGO LA MBUYU
Na. Sylvester Richard.
Mkala – Singida
Masailia ya
mwili likiwemo Fuvu lakichwa linalodhaniwa kuwa ni la mwanamke aitwaye Tabu
Robert, (28), Mkazi waYulansoni, Kata na Tarafa ya Kinyangiri, Wilaya ya
Mkalama, Mkoani Singida ambaye anadaiwa kupotea miaka 8 iliyopita limepatikana likiwa kwenye
pango la mbuyu uliopo umbali wa mita takribani 600 kutoka nymbani kwao.
Akiongea na
Wandishi wa habari hii leo Ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP
Debora D. Magiligimba ameeleza kuwa mnamo tarehe 08.09.2010 Huko katika Kituo
cha Polisi Kinampanda, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida Benard Shumba, (47),
Mnyiramba, Mkulima na Mkazi wa
Kijiji cha Yulansoni alifika Kituoni hapo na kutoa taarifa kuwa Mke wake
aitwaye Tabu Robert, (28), Mkazi wa Yulansoni haonikani nyumbani kwake. Juhudi
za kumtafuta kwa kushirikiana na ndugu zake zilianza bila mafanikio ndipo
alipoendelea kuishi kijijini hapo akitunza mwanae aliyeachwa na Mama yake.
Kamanda
Magiligimba ameeleza kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema liliendelea
kumtafuta ambapo siku ya tarehe 17.03.2018 lilipata taarifa kutoka kwa raia
wema kuwa Tabu Robert hakupotea bali aliuawa na Mme wake ambapo Askari wa Jeshi la Polisi
walifika nyumbani kwa Mtuhumiwa na kufanikiwa
kumkamata, kumhoji na kukiri kufanya mauaji hayo siku ya tarehe
07.09.2010 majira ya saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake na kueleza kuwa baada
ya kutenda kosa hilo aliuchukua mwili wa Marehemu na kwenda kuuficha kwenye mti
wa mbuyu ambao una shimo kubwa na kisha kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi
hicho huku chanzo cha mauaj hayo akieleza kuwa ni ulevi wa pombe za kienyeji wa
Marehemu na kumuacha Mtoto mdogo mwenye
umri wa miaka miwili peke yake kitendo ambacho kimekuwa kero kwa Mtuhumiwa.
Hata hivyo ACP
Magiligimba ameeleza kuwa baada ya mahojiano, siku ya tarehe 18.03.2018 majira ya saa 10:00 jioni Jeshi la
Polisi kwa kushirikiana na Wananchi walifika eneo la tukio ambalo lipo umbali
wa Mita 600 kutoka nyumbani kwa Mtuhumiwa
na kukuta masalia ya mifupa, fuvu na mbavu zidhaniwazo kuwa ni za
binadamu ndipo Askari Polisi walipochuka
sampuli za mabaki hayo kwa uchunguzi zaidi na mabaki mengine kukabidhiwa kwa Ndugu wa Marehemu kwa hatua za mzishi.
Kuhusiana na
tukio hilo Magiligimba amtanabaisha kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia
mtuhumiwa Benard s/o Shumba kwa uchunguzi zaidi na baada ya uchunguzi
kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili ambapo ametoa
wito kwa Wananchi wote
wa Mkoa wa Singida kuendelea kutoa Taarifa zitakazosaidia kuwabaini wahalifu
katika maeneo yao ili kuzidi kutokomeza uhalifu Mkoani Singida pia kuacha
tabia za kujichukulia sheria mkononi pindi wanapokuwa na migogoro ya aina
yoyote bali watoe taarifa kwa viongozi wa Serikali za Mitaa au katika vituo vya
Polisi vilivyokaribu na wao ili matatizo yao yatatuliwe kisheria
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida akijadili jambo na waandishi wa habari leo
hii muda mfupi baada ya kotoa taarifa kuhusu masalia yanayosadikiwa kuwa
ni ya Mwanamke aliyepotea takribani miaka 8 iliyopita. .
Picha ya Raia mwema akiingia katika pango la mti aina ya Mbuyu ili kutoa masalia ya mwili wa binadamu anayesadikiwa kutupwa humo baada ya kuuwa
Picha ya Mti aina ya Mbuyu ambao ndani ya pango lake kuna masalia ya mwili wa Binadamu anayesadikiwa kutupwa humo baada ya kuuwa
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Namba yetu ya WhatsApp 0629 655814
Facebook - machibya richard.
No comments