Watu watano wamefariki dunia na wengine wawili
kujeruhiwa Mkoani Singida baada ya ajali mbili kutokea katika maeneo na
nyakati tofauti.
Kwa
maoni,ushauri, habari, picha na matangazo wasiliana nasi kwa kupitia anwani zifuatazo’
- simu No.
0768 367 454/Whatspp
0652 683 063
Facebook, Machibya Richard
Na Sylvester Richard.
Singida
Watu watano wamefariki dunia na wengine wawili
kujeruhiwa Mkoani Singida baada ya ajali mbili kutokea katika maeneo na
nyakati tofauti.
Akiongea na waandishi wa habari katika Ofisi
yake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi (ACP)
Thobias G. Sedoyeka amesema kuwa ajali zote zimetokea
terehe 14.07.2016 ambapo ajali ya kwanza imetokea
majira ya saa 03:45 usiku huko katika
maeneo ya Tambukareli, Kata, Tarafa na
Wilaya ya Manyoni katika barabara kuu
ya Manyoni- Dodoma ambapo Jofrey Msengeni, (46) Mpogoro Mkazi wa Dar es salaam
akiendesha gari No. T.373 BAP/T.703 AFR
SCANIA TANK inayomilikiwa na Kampuni ya PETROL AFRICA akitokea Dar es salaam - Kahama
akiwa amepakia mafuta aina ya petrol aligongana na gari No. T. 159 AZX TOYOTA
NOAH iliyokuwa ikiendeshwa na Adam Seif, (63), Mwarabu, Mkazi wa Manyoni mjini
na kusababisha vifo vya abiria wawili na
majeruhi wawili ndani ya Noah.
Kamanda
Sedoyeka aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni ahamed Musa, (65), Mwarabu, Mkulima wa
Kintinku Manyoni na Said s/o Arafati, (30), Mwarabu, Mfanyabiashara na mkazi wa
Dodoma mjini na waliojeruhiwa ni Adam Seif, (63), Mfanyabiashara, Mkazi wa
Manyoni mjini, amepata majeraha kichwani, mikono yote na mgongo na Abdallah
Mohamed, (62), Mwarabu, Mfanyabiashara wa Manyoni mjini, amepata majeraha
kichwani na kavunjika mbavu. Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya
ya Manyoni hali zao ni mbaya hali kadhalika Miili ya marehemu imehifadhiwa
hospitalini hapo ikisubiri taratibu za
mazishi.
Aidha katika ajali ya pili Kamanda Sedoyeka
alisema kuwa ilitokea majira ya saa 1:00 usiku huko maeneo ya Muhalala na Kata Muhalala,
Tarafa na Wilaya ya Manyoni, ambapo Gari
No. T.163 BASI SCANIA MALI YA Kampuni ya
OSAKA likitokea Musoma - Dar es salaam
likiendeshwa na Leo s/o Kariwa likiteremka Mlima Muhalala liliwagonga watu
watatu waliokuwa wakitoa msaada katika gari NO T.490 BDX/T591 BCV SCANIA
lililokuwa limeshaharibika na kuwasababishia vifo vyao papo hapo. Basi hilo pia
kutokana na kukosa mwelekeo liliigonga gari NO. T432 BDU Mitsubishi Fuso ikiendeshwa
na Mwanga s/o Kasomo, (35), mgogo, mkazi wa kinanga manyoni ikipandisha mlima
na kusababishia kupinduka na basi kuacha njia na kugonga jiwe.
ACP Sedoyeka
alieleza kuwa waliofariki katika ajali
hiyo ni: Charles s/o Mesomapya, (52), mgogo, Juma s/o Mbonje, (43), msukuma na Adam s/o Sadik, (36), wote wakulima na wakazi
wa Muhalala ambapo Miili yao imehifadhiwa hospitali ya Manyoni ikisubiri taratibu za
mazishi na kuongeza kuwa kuhusiana na ajali hiyo hakuna mtu/watu wanaoshikiliwa kwani madereva
walitoroka baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo Jeshi la Polisi linawatafuta
ili wakamatwe na kufikishwa Mahakamani.
Kamanda Sedoyeka hakusita kutoa wito kwa
madereva wote na watumiaji wengine wa barabara kwa kuwataka kuendesha vyombo
vyao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabrani pia
aliwaasa madereva kukagua magari yao mara kwa mara ili kubaini ubovu wa magari
yao na kurekabisha hivyo kuepuka ajali zisizokuwa za lazima.
Katika mikakati ya kupunguza ajali, ACP
Sedoyeka alisema kuwa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa itakutana ili kuweza kujadili na kupata uvumbuzi wa
kulitatua tatizo la ajali katika Mkoa wa Singida.
No comments