Dereva wa Basi la City Boys afikishwa mahakamani kwa mara nyingine, Dhamana yake bado ni kitendawili kwa kuhofia usalama wa maisha yake.
simu No. 0768 367454
0652 683063
Facebook. Machibya Richard.
Na. Jenister Zedekia
SINGIDA
Mtuhumiwa
anayekabiliwa na mashitaka 30 ya kuua bila kukusudia katika ajali ya Mabasi ya
Cityboys iliyotokea mnamo Julai,04 mwaka huu amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Singida ikiwa ni siku ya
pili tangu amekamatwa ili kujibu tuhuma zinazomkabali.
Awali akisoma shitaka linalomkabili Wakili wa Serikali mwandamizi Seif Ahamed amesema kuwa
mtuhumiwa anakabiliwa na mashitaka 30 ya kuua bila kukusudia kataika ajali ya
mabasi ya Kampuni ya City Boys iliyotokea mnamo julai,4 mwaka huu katika Kijiji
cha Maweni, Kata ya Kitinku, Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida.
Aidha Ahamed
ameeleza kuwa kesi hiyo ambayo ipo katika mahakama ya wilaya ya Singida chini
ya usimamizi wa Hakimu Joyce Minde ambapo kutokana na dharura ya Hakimu huyo na
leo imesikilizwa na Hakimu Frolence Tesha huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha dhamana haitolewi kwa mtuhumiwa huyo.
Pia amesema
kuwa kutokana na Jeremiah Martin amabaye ni mtuhumiwa kutenda kosa la kuua bila
kukusudia ambapo ni kosa na kinyume cha sheria kifungu no.195 na 198 sura ya 16
ujazo 1 ya mwaka 2002.
Sambamba na
hayo Mahakama inajadili juu ya mtuhumiwa kuachiwa kwa dhamana ambapo
inasemekana mtuhumiwa akiachiwa kwa dhamana anaweza kutoroka au kupoteza maisha
kutokana na wananchi kuwa na asira naye.
Hata hivyo
kesi hiyo imeahirishwa hadi mnamo Agosti,01 mwaka huu itakapotajwa tena na
Mtuhumiwa amerudishwa rumande.
No comments