Wananchi wa Singida
waaungana na Watanzania wengine katika kuadhimisha siku ya Mashujaa.
Kama una habari, maoni,
ushauri, matangazo na picha, tuma kupitia anwani zifuatazo;
Email - Sylvestermac87@gmail.com
-
Facebook – Machibya Richard
-
Sim no. 0768 367 454
-
0652 683 063
Na Sylvester Richard.
Singida.
Kila mwaka inapofika
tarehe 25.Julai Nchini Tanzania
hufanyika maadhimisho ya kuwakumbuka Mashujaa waliopigana vita mbalimbali. Mwaka
2016 maadhimisho hayo Kitaifa
yamefanyika Mkoani Dodoma.
Hapo awali
maadhimisho hayo yalikuwa yakifanyika siku ya tarehe 1. Sept. kila mwaka ambapo
baada ya vita vya Kagera mwaka 1978 -
1979 ilihamishiwa Tar. 25. Julai siku ambayo Mashujaa walipokelewa baada ya
ushindi mkubwa dhidi ya Majeshi ya Dhalim na Dikteta Idd Amin Dadaa .
Katika Mkoa wa
Singida Maadhimisho hayo yamefanyika ki Mkoa Wilayani Manyoni huku Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa
Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe.
Akiongea na wananchi
wa Singida katika hotuba yake Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa maadhimisho hayo
hufanyika kila mwaka ili kuwakumbuka Mashujaa waliopigana vita vikuu vya dunia
ambapo vita ya kwanza ilikuwa mwaka 1914 – 1918 na vita ya pili ya Dunia mwaka 1939 – 1945.
Amewataja mashujaa
wengine kuwa ni wale waliopigana katika ukombozi wa Nchi ya Tanzania kupigania uhuru na wengine walipigana
vita vya uvamizi wa Nduli Idd Amini Dadaa wa Uganda.
Mtigumwe aliwataja
baadhi ya Mashujaa wanaokumbukwa kuwa ni pamoja na Mtwa Mkwawa wa Iringa ,
Kinjikitile Ngwale, Mtemi Mirambo na
Isike wa Tabora, All Bushiri Bin Salum
na Kimweri wa Tanga.
Katika kupigania
uhuru wa Nchi ya Tanganyika na Zanzibar, Mtigumwe amewataja Mashujaa waasisi wa
Mataifa hayo ambao ni Mwl Julius
Kambarage Nyerere Rais wa kwanza wa Tanganyika na Hayati Abeid Karume Rais wa
kwanza wa Zanzibar ndiyo walioongoza mapambano dhidi ya wakoloni na hatimaye
Nchi hizo kujinyakulia uhuru.
Kwa kupitia
maadhimisho hayo, Mhandisi Mtigumwe amewaasa wananchi wa Singida kuitunza tunu
ya amani ambayo ni mbegu iliyopandwa na mashujaa hao na maadhimisho hayo ni
ishara ya kuwaenzi na kuwathamini mashujaa wote walio hai na waliotangulia
mbele ya haki.
Kisha Mtigumwe alitoa
wito kwa wananchi wote kwa ujumla kutoa michango yao katika ulinzi na usalama
wa Nchi ya Tanzania kwa kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani kwa vyombo
vya ulinzi na usalama ili viweze kuthibitiwa mapema.
Picha wapi
ReplyDeletePicha wapi
ReplyDelete