-
Facebook – Machibya Richard
-
Sim no. 0768 367 454
-
0652 683 063
Hizi ni picha za maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika Mkoani Singida katika Wilaya ya Manyoni siku ya tarehe 25.07.2016. Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Nchini Tanzania kila inapofika tarehe 25 Julai kuwakumbuka Mashujaa waliopigana vita mbalimbali vikiwemo vita vya Dunia na vya ukombozi wa Nchi hiyo kutoka mikononi mwa wakoloni na hatimaye kujipatia Uhuru na vita vya Kagera ambavyo vilipiganwa baada ya miaka 17 tangu Tanganyika ilipopata Uhuru.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akikaribishwa kukagua gwaride lililoandaliwa kwa ajiri ya maadhimisho ya siku ya
Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika uwanja wa Halimashauri ya Wilaya ya
Manyoni Mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajiri ya maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika uwanja wa Halimashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiweka mkuki kwenye mnara
wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika uwanja wa Halimashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Thobias G.Sedoyeka akiweka silaha ya jadi kwenye mnara
wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika uwanja wa Halimashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
Afisa tawala Mkoa wa Singida Dkt. Anjelina Lutambi akiweka shada la maua kwenye mnara
wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika uwanja wa Halimashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe akiweka mkuki kwenye mnara
wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika uwanja wa Halimashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
No comments