Dhamana ya Watuhumia
wanaokabiliwa na makosa 30 ya kuua bila
kukusudia katika ajali ya mabasi ya City Boys yawa gumzo.
Kwa matangazo, habari, picha na ushauri, wasiliana nasi kwa kupitia anwani zifuatazo;
sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768 - 367454/0652 683063
Facebook - Machibya Richard.
Na Jenista Zedekia.
Singida.
Watuhumia
wanaokabiliwa na makosa 30 ya kuua bila
kukusudia katika ajali ya mabasi ya City Boys iliyosababisha vifo vya watu 30
na majeruhi zaidi ya Hamsini dhamana kwao imekuwa gumzo kutokana na mazingira ya kesi hiyo.
Akisoma
mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida Wakili wa
Serikali Bi.Petrida Muta amesema kuwa watuhumiwa wote wawili Jeremiah Martin
(34) na Boniphas Douglas (37) hawatakiwi kupewa dhamana kutokana na mazingira
ya kesi inayowakabili.
Bw.Fransis
Kitope ambaye pia ni wakili kwa upande
wa utetezi ameiomba mahakama hiyo kuweza kujadiliana kwa maneno juu ya
watuhumia hao kupewa dhamana kwani ni haki yao huku akisema kuwa dhamana
haiwezi tolewa kwa mtuhumiwa mmoja.
Aidha Hakimu
mkazi wa Mahakama hiyo Joyce Minde amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na utakapokamilika watuhumiwa
wote wawili watatiwa hatiani kwa makosa ya kuua bila kukusudia kinyume na
kifungu cha 195 na 198 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2002.
Hata hivyo
kesi imehahirishwa hadi Augost,04,mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuzungumza
kwa maneno kwa upande wa mwendesha mashitaka na kwa upande wa utetezi na
watuhumiwa wamerudishwa rumande.
No comments