RC Singida
amwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Manyoni
Kwa maoni,ushauri,
habari, picha na matangazo tuma kwa kupitia anwani zifuatazo’
- simu No. 0768
367 454/Whatspp
0652 683 063
Facebook, Machibya Richard
Na Sylvester Richard.
Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi
Mathew Mtigumwe amemwapisha Mkuu wa
Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe
ambaye alikuwa safari wakati wakuu wa wilaya wengine wanne wakiapishwa
siku ya terehe 01.07.2016 .
Akiongea muda fupi baada ya
kumwapisha Mkuu wa Wilaya huyo, Mhandisi Mtigumwe alimuasa kwenda kufanya kazi
kwa uadilifu mkubwa katika kusimamia
wafanyakazi ili kuweza kuwatumikia wananchi vizuri na kuleta maendeleo stahiki
ikiwa ni pamoja na kusimamia mapato ili mapato hayo yalete maendeleo kwa kukusanya kodi kupitia wafanyabiashara wenye leseni halali . Alimtaka
Mkuu wa Wilaya huyo kwenda Kusimaia halimashauri ili zikae na mamlaka ya mapato
ili zifanye kazi kama timu badala ya kila mmoja kufanya kazi kivyake.
Mhandisi Mtigumwe alimtaka kwenda
kusikiliza kero za wananchi kwani kuna
watendaji wanaofanyakazi kwa mazoea kama Miungu Watu na kusema kuwa tatizo hilo linatakiwa liondolewe ili Singida
iwe mfano mzuri kwa maendeleo chanya.
Kuhusiana na miradi alieleza kuwa kuna
miradi ambayo inatelekelezwa ambapo katika aslimia 40 ya bajeti ya mwaka ni miradi, kuna miradi ambayo
inatekelezwa kwenye ngazi ya Wilaya na katika Halimashauri zetu, lazima isimamiwe
vizuri kwani ofisi za Wakuu wa Wiliaya
ndizo zitatumika moja kwa moja katika kuangali
Mirada inatekelezwaje.
Kuhusu tatizo la watumishi hewa
Mhandi Mtigumwe alieleza kuwa zoezik hilo ni endelevu kwani linajitokeza mara
kwa mara kwa hiyo mtu anapostaafu, kuachishwa kazi au kufarika lazima aondokewe
kwenye daftari la malipo maramoja.
Akiongea kuhusu suala la madawati
alimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa wilaya ya
Mnyoni ilikuwwa ya mwisho katika kukamilisha zoezi hilo na kumtaka alisimamie
hilo ili kufikia tarehe 15.06.2016 wilaya yake iwe imekamilisha zoezi hilo ambapo
Mkoa mzima utakuwa umekamilisha na kuongeza kuwa baada ya madawati zoezi litahamia kwenye madarasa
na maabara ambapo kitaandaliwa kikao cha elimu kwa ujumla ambacho
kitashirirkisha wadau wa elimu wote ili kuweza kujadiliana maswala yanayohusu
elimu kwani Mkoa wa Singida umekuwa wa 18 katika matokeo ya kidato cha nne ambapo
kikao hicho kitapanga namna ya kuongeza juhudi na kupiga hatua kubwa katika
kuboresha elimu.
Kuhusu kilimo Mkuu wa Mkoa alieleza
kuwa kutokana na Mkoa wa Singida kuwa na Mvua chache alimtaka Mkuu wa Wilaya ya
Manyoni kwenda kuwahamasisha wananchi
kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwa ni pamoja na kuanzisha maeneo ya masoko ili mkulima asiuze mazao yake
nyumbani bali apeleke katika soko ambapo Halimashauri inaweza kukusanya mapato
yake.
Mhandisi Mtigumwe alimalizia kwa
kusema kuwa tangu tarehe 01.07.2016 mchakamchaka wa kusaka maendeleo kwa kasi umeanza na hivyo alimtaka Mkuu wa wilaya kutokusita kumchuklulian hatua mtu yeyote
atakayekwamisha shughuli nzima ya kuleta maendeleo katika Mkoa wa Singida na
Nchi nzima kwa ujumla.
No comments