Mbunge Tundu Lisu akamatwa
na Jeshi la Polisi baada ya hotuba yake Ikungi mkoani Singida.
Tuma maoni,
ushauri, habari na picha kuptia
E,mail – sylvestermac87@gmail.com
-
Facebook Machibya Richard
-
Sim 0768 367454
-
0652 683063
Na. Sylvester
Richard
Singida
Mbunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Tundu
Lisu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kutoa maneno ya kichochezi.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Wa Polisi (ACP) Thobias G. Sedoyeka amesema kuwa Mbunge Tundu Lisu
alitoa maneno ya uchochezi wakati akihotubia katika mkutano wake na wananchi wa Jimbo la Ikungi Mashariki tarehe 03/08/2016.ambapo mkutano ulianza majira
ya saa 9:45 alasiri na kumalizika majira ya saa
12:20.
Aidha ACP Sedoyeka ameeleza kuwa katika mkutano huo Mbunge huyo alitoa
maneno ya uchochezi kwamba tarehe 1.09.2016 watu wote wajitokeze kufanya
mikutano Nchi nzima bila uoga kuunga mkono kaulimbiu ya Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (UKUTA) na kwamba Rais Magufuli hana mamlaka yoyote ya
kuwazuia kufanya mikutano hiyo huku akidai kuwa jukumu hilo ni la Mkuu wa
Polisi Wilaya husika peke yake.
Hata hivyo Mh. Mbunge Tundu Lisu anakesi ya kujibu kuhusiana kosa la Kutoa
lugha ya uchochezi huko Dar-es-Salaam lililopelekea kufunguliwa jalada namba CD/IR/5962/2016 katika kituo cha Polisi Kati jijini
Dar-es-Salaam alisema Kamanda Sedoyka.
Katika hatua nyingine tena ACP Sedoyeka akaeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa
kina kwenye mitandao ya kijamii kufuatia ujumbe mfupi wa maneno uliosambazwa
katika mitandao hiyo baada ya kukamatwa kwa Mh. Tundu Lisu ukiwa na ishara zote za uchochezi uliosomeka
kama ifuatavyo nanukuu ‘Breaking
news!!!!! wakubwa sana salaam.
Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa Polisi Singida.
nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao
makuu ya jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani
nimefuatwa Region Crime Officer wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina
la BABU MOLLEL na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Reginal Police Commander Singida
nikamatwe. Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar-es-Salaam. kwahiyo
niko nguvuni ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. Its
likely nitasafirishwa Dar usiku huu. Infact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi.
Kwa vyovyote itakavyokuwa, there is no turning back. There is no shutting up. Nitapambana
kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom
or in jail, as long as I’have a voice to speak with. Sitakubali kunyamaziswa na
Dikteta uchwara. Msikubali kunyamazishwa na Dikteta Uchwara. Aluta
continua!!!!!! From Tundu Lisu.’ . Katika uchunguzi huo endapo atabainika mtu
yoyote kutuma taarifa hiyo basi Jeshi la
Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria zinazostahili ikiwemo kuwakamata na kuwafikisha mahakamani
mara moja.
Kamanda Sedoyeka alisema kuwa mpaka sasa hivi Mbunge huyo Amesafirishwa Dar es salaam kwa uchunguzi zaidi na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani na kisha akatoa wito kwa wananchi kuacha kutoa lugha yoyote
yenye ishara ya kichochezi inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani katika Nchi
yetu kwani kufanya hivyo kinyume cha sheria na hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
No comments