Angalia hapa picha za wananchi wa Mkoa wa Singida wakiwa katika Uwanja wa michezo Namfua wakiliombea Taifa la Tanzania Amani.
Mbele kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwasili katika uwanja wa michezo Namfua uliopo katika Manispaa ya Singida kwa ajiri ya kuwaongoza wananchi wa Mkoa wa Singida Katika kuliombea amani Taifa la Tanzani na Afya njema kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwa katika uwanja wa Michezo Namfua katika shughuli za kuliombea Taifa, Wa tatu kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mh.Elias Tarimo na wanne kutoka kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu mwandamizi wa Polisi (SSP) Mayalla Towo.
Pichani ni kikundi cha Kwaya Kinachojulikana kwa jina la Msifuni Emanuel Kutoka kanisa la KKKT Singida kikiimba nyimbo za kuhamasisha Amani Nchini Tanzania Katika Uwanja wa Namfua uliopo katika Manispaa ya Singida.
Kikundi cha kwaya Kutoka Dhehebu la S.D.A Unyankindi Mkoani Singida kikiimba kuhamasisha amani Nchini Tanzania katika Uwanja wa Namfua uliopo katika Manispaa ya Singida.
Kwaya ya Mabalozi wa Yesu kutoka Kanisa la T.A.G Singida ikiimba kuhamasisha amani Nchini Tanzania katika Uwanja wa Namfua uliopo katika Manispaa ya Singida.
Katikati aliyeshika kipaza sauti ni Shekhe Issa Nassoro akiongoza maombi kuliombea Taifa la Tanzania Amani pamoja na kuomba baraka kwa michango iliyokusanywa kwaajiri ya waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
Mtoto Yusuph Mohamed Nassoro akitoa Mchango kwaajri ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la Ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu na uharibifu wa baadhi ya nyumba pamoja na miundombinu.
Mkuu wa Mkoa Mhandisi Mathew Mtigumwe akisalimiana na wachezaji wa timu ya Taasisi za Kidini na timu ya muungano wa wazee wa Manispaa ya Singida muda mfupi kabla ya shughli ya maombezi kuanza katika Uwanja wa Namfua Manispaa ya Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida akisalimiana na waamuzi wa pambano la mpira wa miguu kati ya Timu ya taasisi za kidini na muungano wa wazee Singida. Waamuzi hawa wote ni wakike.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Myalla Towo akwasalimia wachezaji wa Mpira wa miguu katika Uwanja wa Namfua katika Manispaa ya Singida muda mfupi kabla ya shughuli ya maombezi kuanza katika Uwanja wa Namfua Manispaa ya Singida.
Mwananchi Joseph Ndimira Mkazi wa Singida aliyesimama kulia akijitolea kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye mahitaji ya damu katika Hospitali mbalimbali Nchini Tanzania.
No comments