Breaking News





Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe awaongoza wananchi wa Singida katika kuliombea Amani Taifa la Tanzani.




  
Kama una habari, matangazo na  picha wasiliana nasi kwa kupitia anwani zifuatazo;
            -  machibya.richard@yahoo.com
Facebook – Machibya Richard
Sim No.  – 0768 367 454
               - 0652 683063

Na.Sylvester Richard

Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe amewaongoza wananchi wa Mkoa wa Singida waliohudhuria katika Uwanja wa Namfua uliopo katika Maspaa ya Singida kwa ajiri ya kuliombea amani Taifa la Tanzani, Kumuombea afya njema  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli na Kuchangia michango kwa ajiri ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Aidha tukio hilo la kihistoria limefanyika leo tarehe 26.10.2016 kuanzia majira saa 5:00 asubuhi na kuhudhuriwa na   wananchi katoka dini na madhehubu mbalimbali wakiwemo wachungaji, Mapadre na Mashehe ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida ndiye mgeni rasmi.  

Katika hotuba yake Mhandisi Mtigumwe amewapongeza wananchi wa Singida kwa kupanga na kufanikisha shuguli hiyo ambayo imeweza kufanikisha maombi na kukusanya michango kiasi cha Tsh. 4,344,450/= kati ya kiwango hicho  pesa taslimu  kiasi cha 2,584,450/= na 1,760000/= ni  ahadi pamoja na mifuko mitatu ya nguo vitu ambavyo vitapelekwa kwa wathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni Mkoani wa Kagera.

Amewahamasisha viongozi wa dini kuendelea kuiombea Nchi na kitendo hicho cha kukutana kwa pamoja kwa ajiri ya maombi bila kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini, siasa, rangi, jinsia na ukanda kifanyike kila mwaka ili Tanzania iendelee kuwa na  amani  kwani ndiyo wajibu wao ambapo pia amewaasa wanachi kulinda amani iliyopo sasa.

Hata hivyo Mtigumwe amewataka wananchi wa Mkoa huo kudumisha  mshikamano ili  kuharakisha maendeleo ya Mkoa na Nchi kwa ujumla na kutoa wito kwa wale wanaovunja sheria za Nchi kuacha mara moja kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale watakaobainika kuzivunja sheria hizo.









No comments