Kama una habari, matangazo, picha na maoni, wasiliana nasi kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail -sylvestermac87@gmail.com
- machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768 367 454/0652 683 063
-Whats app 0768 367 454
- Facebook Machibya Richard.
SSP Mayalla Towo Kaimu Eneo la machimbo lililopo
Kamanda wa Polisi (M) Singida Kijiji cha Mgongo Singida.
Na.
Sylvester Richard.
SINGIDA.
Watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa Mkoani
Singida baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo wakiwa wanachimba madini ya
Dhahabu katika eneo la machimbo lijulikanalo kwa jina la ZAMBIA
lililopo katika Kitongoji, Kijiji na Kata
ya Mgongo, Tarafa ya Sheluhi, Wilayani Iramba.
Akiongea na waandishi wa
Habari Ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu
mwandamizi wa Polisi (SSP) Mayalla Towo
ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 02/11/2016 majira ya saa 7:40
mchana na kuwataja waliofariki dunia kuwa ni Anna Martine, (56), Paulina Msengi, (45) na Magreth Samwel, (45) wote Wanyiramba, Wakulima/Wachimbaji wa madini wadogo wadogo
wakazi wa Kijiji cha Mgongo ambapo waliojeruhiwa ni Amri Hamisi, (34) na Sambo Msengi,(16) .
Kaimu Kamanda ameeleza
kuwa Jeshi la Polisi lilipopata taarifa kuhusiana na tukio hilo ambapo yeye mwenyewe akiongozana na askari
wengine kutoka kitengo cha upelelezin walifika eneo la tukio kufanya uchunguzi
wa awali na kubaini chanzo cha ajali hiyo kuwa ni wachimbaji hao kushindwa
kuchukua tahadhari wakati wakifanya shughuli zao za uchimbaji.
Aidha alisema kuwa Majeruhi
wote wamelazwa katika kituo cha afya cha Mgongo na hali zao zinaendelea
vizuri ambapo miili ya marehemu
imefanyiwa uchunguzi wa Daktari na
kukabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za mazishi.
Kaimu Kamanda lichukua nafasi hiyo kutoa wito kwa wachimbji wadogo
wadogo kuwa wanatakiwa kuchukua tahadhari kubwa wakati wanaingia katika
machimbo hayo ili kuhakikisha kuwa hakuna dalili yoyote yenye kuhatarisha
maisha yao.
No comments