Waandishi wa habari Singida waaswa kuwapa habari sahihi wananchi ili wajue wajibu na nafasi yao katika kupambana kuleta maendeleo ya Mkoa wa Singida na Nchi ya Tanzania kwa ujumla.
Na
Sylvester Richard.
SINGIDA.
Afisa Tawala Wilaya ya Singida Mh. Wilisoni Shimo amewaasa
waandishi wa habari wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Singida
(SINGPRESS) kuwapa habari sahihi Wananchi ili
wajue wajibu na nafasi yao
katika kupambana kuleta maendeleo katika
Mkoa wa Singida na Nchi ya Tanzania kwa ujumla.
Mh. Shimo ameyaongea hayo wakati wa hotuba yake
aliyoitoa akiwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Chama Cha Waandishi wa Habari Singida
(SINGPRESS) uliofanyika tarehe 13.May 2017 majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa
KBH Hotel iliyopo kando kando ya ziwa Singidani katika Manispaa ya Singida
Aidha katika Mkutano huo uliolenga kuienzi siku ya
Uhuru wa Habari Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 03 May kila
mwaka ambapo mwaka 2017 imeadhimishwa Kitaifa Mkoani Mwanza huku Mkoa wa
Singida ukiadhimisha tarehe 13.May. Mh. Shimo ametoa pongezi kubwa kwa
Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida kwa
kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya mkoa wa Singida na Nchi Kwa ujumla.
Mh. Shimo amewataka waandishi kuendelea kuandika
habari zenye kuibua uhalifu zikiwemo zile za kupinga uuzaji na utumiaji wa
madawa ya kulevya, ukatili, rushwa, ufisadi, ajali mbalimbali za barabarani na
habari zingine zenye kuleta mwitikio chanya katika kuleta maendeleo ya Nchi.
Alichukua nafasi pia kuwaasa Waandishi wa Habari kuandika Habari sahihi zilizojitoshereza, ambazo hazina
upendeleo ,za kweli, za uhakika zenye kutegemewa na wanasingida na Watanzania
kwa ujumla ili ziwasaidie katika kujua nini kinaendela katika Nchi juu ya maendeleo
na kuachana na habari zenye kuchonganisha na kusababisha kuvuruga amani ya Nchi
na wakati mwingine kusababisha vifo.
Akiongelea kuhusu Uchumi wa Chama cha waandishi wa Habari
Singida (SINGPRESS) Mh. Shimo
amekishauri Chama hicho kuwatumia Waandishi wazuri wabunifu ambao wanaweza kuandika miradi mbalimabli
ambayo SINGPRESS inaweza kuifanya ili wadau wengi waifahamu na hivyo kujitokaeza
kusaidia na kuinua uchumi wa Chama na Waandishi
wa habari mmoja mmoja.
Alitaja Njia nyingine ya kuinua uchumi wa Chama hicho
kuwa ni kuandaa Mihadhara mbalimbali ya mara kwa mara ambayo itawasaidia Wananchi wa Mkoa wa
Singida kuelewa umuhimu wa habari na hivyo kuwa wadau wazuri wa habari.
Akiongea kuhusu changamoto za Chama ( SINGPRESS)
ikiwemo upatikanaji wa Kiwanja kwa ajiri ya Kujenga Ofisi ya chama hicho, Mh.
Shimo amesema kuwa Ofisi yake ipo tayari kuchangia kwa kadiri itakavyowezekana
na kuahidi kuwa atafikisha changamoto hizo katika uongozi wa Mkoa ili kuona jinsi ya kutatua changamoto hizo.
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi (SSP) Issaya Mbughi
ambaye ni mtoa mada katika Mkutano huo amewashukuru wanahabari wa Mkoa
wa Singida kwa kuonesha ushirikiano mkubwa katika kuandika habari zinazosaidia
katika kuielimisha Jamii kuhusu kudumisha amani ya Mkoa na Nchi yote kwa
ujumla.
SSP Mbughi ameeleza kuwa jukumu la usalama wa Nchi ni jukumu la
kila Mtanzania hususani mzalendo wa kweli pia na waandishi watambue kuwa
kuvurugika kwa amani ya nchi hakuna shughuli yoyote ile iwe ya kijamii, Kisisa,
kiuchumi itakayoweza kufanyika, hivyo elimu hii kwa Wananchi ni muhimu sana na
kuongeza kuwa Waandishi wa habari ni wadau muhimu sana katika kufikisha elimu
hii kwa wananchi.
Hata hivyo Kaimu
Kamanda alichukua fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kuandika habari kwa
kuzingatia sheria na kanuni za kiuandishi ambazo zimeainishwa katika Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kufanya hivyo watakuwa wameepuka migogoro
mingi kati yao na Jamii ambayo ndiyo wateja wa kazi zao.
Mwisho Kaimu Kamanda SSP Mbughi akasisitiza
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo isisemayo kuwa
‘Klabu za waaandishi wa habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika
jamii ’ Wakizitumia vizuri kalamu zao tutaienzi Tanzania ambayo ni
kisiwa cha amani.
Pichani ni Afisa Tawala
Wilaya ya Singida Mh. Wilison Shimo akiongea na waandishi wa Habari katika Mkutano wa Waandishi uliofanyika katika Ukumbi wa KBH Hotel iliyopo katika maeneo ya Singidani Manispaa ya Singida.
Mwenyekiti wa Chama cha
waandishi wa Habari Singida (SINGPRESS) Ndugu Ranko Banadi akifungua Mkutano wa waandishi
wa habari katika Ukumbi wa KBH Hoteli.
Kaimu Mwenyekiti wa
SINGPRESS Ndugu Shabani Msangi akichangia mada kwenye Mkutano
wa waandishi wa habari Katika ukumbi wa KBH Hotel Singida.
Katibu wa SINGPRESS
Ndugu Emannueli Michael akitoa mwongozo katika Mkutano wa Waandishi wa Habari
Ukumbi wa KBH Hotel katika Manispaa ya Singida.
Waandishi wa Habari
pamoja na wadau wa habari wakifuatlia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na
mmoja wa washiriki wa Mkutano katika Ukumbi wa KBH Hotel Manispaa ya Singida
Kaimu Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoa wa Singida SSP Isaya Mbughi akitoa Mada katika Mkutano wa waandishi wa Habari Singida katika Ukumbi wa KBH Hoteli Manispaa ya Singida.
Pichani ni Mkurugenzi
wa MACHIBYA BLOG Ndugu Sylvester Richard akifuatilia Mada iliyokuwa ikitolewa na mmoja wa watoa mada
kwenye Mkutano wa waandishi wa Habari katika ukumbi wa KBH Hotel Manispaa ya
Singida.
Mmoja wa wadau wa habari akichangia mada katika
Mkutano wa waandishi wa Habari Singida katika Ukumbi wa KBH Hoteli Manispaa ya Singida.
Mkutano wa waandishi wa Habari Singida katika Ukumbi wa KBH Hoteli Manispaa ya Singida.
Pichani wa tatu kutoka kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Singida Mh. Wilison Shimo akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wawakililishi wa vyombo mbalimbali vya habari, wanachama na
wadau wa habari waliohudhuria katika Mkutano wa waandishi uliofanyika katika
Ukumbi wa KBH Hotel katika Manispaa ya Singida.
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Namba yetu ya WhatsApp 0629 655814
Facebook - machibya richard.
No comments