Pichani ni Kamanda wa Polisi Mko wa Singida Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Debora Magiligimba akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake.
Watu wawili
wamefarikidunia Mkoani Singida baada ya kukanyagwa na wanyama jamii ya Tembo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina
Msaidizi wa Polisi (ACP) Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa vifo
hivyo viliyosababishwa na wanyama hao wakubwa Duniani waliokadiri kuwa katika kundi
la Tembo 32 waliovamia maeneo ya Kitongoji cha Italala katika Kijiji cha
Musimi, Kata na Tarafa ya Sepuka Wilayani Ikungi siku ya tarehe 04.05.2017
majira ya saa 4:00 asubuhi.
Kamanda
Magiligimba amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na Hassan s/o Shaban @ngabu,
Mnyaturu (68), Mkulima wa Italala
aliyekuwa akiendelea na shughuli za kuvuna mahindi ambaye alishambuliwa
na Tembo hao kwa kumrusha juu na kumkanyaga kanyaga sehemu mbalimbali za mwili
wake na kumsababishia Kifo cheke papo hapo.
Mwingine amemtaja
kuwa ni Ayoub s/o Emmanuel,Mnyaturu, (19), ambaye alikuwa akiwashangaa Tembo
hao akiwa amepanda juu ya mti ambapo Tembo hao walivunja tawi la Mti na kuanguka chini
na kupata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake ndipo alikimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa
Singida na ilipofika majira ya saa 10 :00 jioni alifariki Dunia.
Hata hivyo
Kamanda ameeleza kuwa imebainika wanyama hao wanatabia ya kupita maeneo hayo
mara kwa mara lakini ni kwa muda mrefu hawajapita maeneo hayo na imebainika
kuwa mara ya mwisho walipita mwaka 1974.
Magiligimba
hakusita kuchukua fursa hiyo kutoa wito kwa Wananchi wa Singida na kuwataka
kutoa taarifa kwa haraka kwa vyombo vinavyohusika na uhifadhi wa wanyamapori
ili kuchukua tahadhari mapema kabla madhara hayajatokea.
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Namba yetu ya WhatsApp 0629 655814
Facebook - machibya richard.
No comments