Breaking News

Mtu mmoja ashikiliwa na Polisi Mkoani Singida kwa kupatikana na Mirungi na wengine wawili kwa kuuza petroli kinyume cha sheria.




WATU WATATU WASHIKILIWA MKOANI SINGIDA KWA MAKOSA MAWILI TOFAUTI



SINGIDA.

Jeshi la Polisi Mkoani Singida linawashikilia watu watatu kutokana na matukio mawili yaliyojitokeza semu na nyakati tofauti.



Akiongea na waandishi wa habari hivi jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi wa Polisi  (ACP) Debora  D. Magiligimba ameeleza kuwa tukio la kwanza ni tukio la ukamatwaji wa mtuhumiwa anayejihusisha biashara ya dawa za kulevya ain ya mirungi aitwaye Haji Yahaya, (28), Muha, Dereva na Mkazi wa Mwanza.



Kamanda Magiligimba amaeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi siku ya tarehe 21. 08. 2017 majira ya saa 8:00 mchana akiwa kwenye gari Na. T.250 BEQ BUS mali ya Kampuni ya ABOOD akitokea Mwanza kwenda Dar es salaam ambapo Jeshi la Polisi lilipata taarifa hizo ndipo Basi hilo lilipofika Mkoani Singida lilikamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Singida na kufanyiwa upekuzi ambapo katika upekuzi huo lilipatikana begi la Mtuhumiwa lililokuwa na mirungi bunda 24 ambayo ni sawa na Kg. 12 ndani yake likiwa limehifadhiwa kwenye buti.



Aidha ACP Magiligimba amaesema kuwa Mtuhimwa  anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano ili kufahamu mtandao wote anaoshirikiana nao katika biashara hiyo ili nao wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Kamnda amechukua nafasi hiyo pia kuwataka wananchi wote wa Mkoa wa Singida na Nchi  kwa ujumla kuachana na biashara ya dawa za kulevya ambayo ni kinyume cha sheria za Nchi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea na misako mbalimbali ya kubaini mitandao inayojihusisha na dawa za kulevya na uhalifu mwengine wenye dalili ya kuvunja amani ya Nchi.



Katika tukio la pili ACP Magiligimba ameeleza kuwa ni tukio la kuungua moto kwa nyumba ya Asheri James,(67) Mnyiramba, Mkulima na mkazi wa Veta – Stesheni ambapo ameeleza kuwa katika ajali hiyo ambayo ilitokea siku ya tarehe 22.08.2017 majira ya saa 2:15 usiku  watu wawili ambao ni Rashid Omari, (45), na Hawa Shabani, (32),  wanandoa na wapangaji katika nyumba hiyo wameungua sehemu mbalimbali za miili yao.





Magiligimba ametanabaisha kuwa chanzo cha moto huo ni dumu lililokuwa na mafuta ya petrol kushika moto na kwamba wanandoa hao wana duka lao katika nyumba hiyo ambamo wanauza bidhaa mchanganyiko ikiwemo mafuta ya petrol ambapo siku ya tukio alifika mteja akihitaji petrol Lita moja na kuhudumiwa na Hawa Shabani hivyo wakati akirudisha dumu lililokuwa na Petrol  ndani likiwa halijafunikwa alilipitisha karibu na mshumaa uliokuwa ukiwaka ndipo moto ulipolipuka na kuliunguza dumu hilo na moto kushika nguo za Hawa Shabani na kuungua zote. Katika harakati za kumwokoa Mke wake Rashid Omari naye aliungua kisha moto kusambaa katika vyumba vingine.



Ameeleza kuwa kuhusiana ajali hiyo Jeshi la Polisi linawashikilia wanandoa hao huku wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa Singida kwa kosa la kufanya biahsara ya Petrol mahali ambapo siyo halali kwa biashara hiyo.



 ACP Magiligimba ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kuacha kufanya biashara ya petrol na nishati zingine zinazofanana na hizo katika maeneo yasiyo rasmi kwa biashara  hizo ili kuepukana na majanga ya moto yanayosababishwa na nishati hizo.







Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi wa Polisi  (ACP) Debora  D. Magiligimba akionesha mabunda ya Mirungi kwa waandishi wa habari Ofisini kwake.








Pichani ni Mabunda ya Dawa za kulevya aina ya Mirungi yaliyokamatwa Mkoani singida.

Kama una Habari., Matangazo, Picha, Maoni na ushauri , tuma kupitia anwani zifuatazo;
E-mail sylvestermac87@gmail.com/machibya.richard@yahoo.com
Sim no . 0768367454/0652683063 . WhatsApp 0629655814


















No comments