JESHI LA POLISI MKOANI SINGIDA LAFANIKIWA KUKAMATA DAWA ZA KULEVYA
JESHI LA
POLISI MKOANI SINGIDA LAFANIKIWA KUKAMATA DAWA ZA KULEVYA
SINGIDA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limefanikiwa
kuwakamata Watu watatu ambao wanajihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa
zakulevya aina ya Bhangi na Heroin.
Akiongea na Waandishi wa habari
Ofisini kwake hii leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora D.
Magiligimba ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na operation ya kupambana na dawa za kulevya Nchini
ambayo ni endelevu ambapo Jeshi la
Polisi Mkoa wa Singida kwa nyakati tofauti Mwezi Desemba 2017 limefanikiwa
kukamata Dawa za Kulevya aina ya Bhangi Misokoto 238 sawa na
gms 484 ambapo watuhumiwa watatu Jeremiah Yombo @Magaja, (53),
Msukuma,Mkulima na mkazi wa manyoni,
Daud Salum, (24), Mkulima, Mnyaturu, Mkazi wa Ukombozi na Hamis Ramadhani, (27), Mnyaturu, Mkulima na mkazi
wa Ginery huku Mtuhumiwa Daud Salum, (24), kwa mara nyingine akikutwa na dawa
za kulevya aina ya Heroine Kete (80) .
Aidha Kamanda Magiligimba
amebainisha mbinu zilizotumika katika kuhifadhi Dawa hizo ni Kuficha ndani ya matundu ya sabufa na kuuza kidogo kidogo pia bangi hizo zilifichwa kwenye begi dogo la
mgongoni kisha begi hilo kupuliziwa pafyumu ili kupoteza harufu ya bangi.
Hata hivyo Magiligimaba ameeleza
kuwa Katika msako huo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata vitu mbalimbali
nyumbani kwa Mtuhumiwa Daud Salum, (24 vikiwa
ni pamoja na Flat screen 1 Nchi 24, sabufa 1 na spika zake 2, Deki 2 aina ya
SONNY, Majiko mawili ya gesi mapya, Mtungi wa gesi kilo 30, Mashuka ya kimasai
mapya 15 na kifaa kimoja kiitwacho Mult sensor aina ya smart vifaa ambavyo vinasadikiwa kuibwa katika
maeneo mbalimbali na kupelekwa pale na watumiaji wa dawa za kulevya ili waweze
kupatiwa herone baada ya kukosa pesa za kununulia dawa za kulevya.
ACP Magiligimba ameeleza kuwa
watuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi kwa mahojiano kabla ya kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili na kutoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Singida kuendelea
kushilikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na
kuwataka wazazi na walezi kuwasisitiza vijana wao kutojihusisha na utumiaji na
uuzaji wa dawa za kulevya. Amewashauri
wananchi kuacha mara moja tabia ya
kununua vitu bila kupewa risiti halali na kutoa wito kwa wanchi walioibiwa vitu
vyao kufika katika Kituo cha Polisi Singida wakiwa na risiti za manunuzi ya
vitu husika ili kuweza kutambua vitu vyao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Debora D. Magiligimba Akionesha radio aina ya Sabufa ambamo zilikuwa zimefichwa Dawa za kulevya aina ya Heroine. Chini ni vitu mbalimbali vilivyopatikana wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida likifanya Oparesheni.
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Namba yetu ya WhatsApp 0629 655814
Facebook - machibya richard.
hongera kwa jeshi la polis mkoni sgd kwa kazi zuri
ReplyDelete