KOCHA WA SINGIDA UNITED AIBIWA MKOBA AKISHANGILIA BAO LA KUONGOZA , JESHI LA POLISI LAFANYA MSAKO MKALI LAFANIKIWA KUUPATA MKOBA, MWIZI ATOROKEA KUSIKOJULIKANA.
KOCHA WA
SINGIDA UNITED AIBIWA MKOBA AKISHANGILIA BAO LA KUONGOZA , JESHI LA POLISI LAFANYA MSAKO MKALI LAFANIKIWA KUUPATA MKOBA, MWIZI ATOROKEA
KUSIKOJULIKANA.
Kocha wa
Timu ya Mpira wa miguu ya Singida United
Johannes
Francis Plugyn, (69), Mholanzi aliibiwa mkoba wake wakati akiungana na
mashabiki na wapenzi wa timu ya Singida united kushangili ushindi wa bao 1- 0
dhidi ya Timu ya Tanzania Prison bao la kuongoza ambalo lilifungwa na Mchezaji
wa timu hiyo Elinywesia Sumbi (Msingida) katika dakika ya sita ya nyongeza baada ya
dakika 90 kumalizika bila kufungana.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Singida Mrakibu
mwandamizi wa Polisi Isaya K. Mbughi akiwa ofisini kwake jana leo amekiri kutokea kwa tukio la kuibwa kwa mkoba
wa Kocha huyo Mahiri.
Mbughi ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira
ya saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Namfua, Kata ya Utemini,
Tarafa ya Mungumaji, Wilaya na Mkoa wa Singida ambapo Johannes Francis Plugyn,
(69), Mholanzi, Kocha wa Timu ya mpira wa miguu ya Singida United akiwa
uwanjani wakati wa kutoka baada ya mechi kumalizika huku baadhi ya Mashabiki wa
Singida United wakimzunguka
wakishangilia ushindi , aliibiwa mkoba aina ya
macron brand uliokuwa na simu
(smart phone) aina ya samsung pro 9 yenye thamani ya usd. 700 sawa na Tshs
1,575,700/=, pochi (wallet) ,leseni za udereva za Nchi mbili ambazo ni Ghana na
Tanzania, pesa taslimu usd 100 sawa na Tshs 225,100/=, Tshs. 200,000/ na funguo za gari.
Hata hivyo Kaimu Kamanda amesema kuwa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Singida lilipata taarifa hizo muda mfupi baada ya tukio hilo na
Msako Mkali ulifanyika kuanzia majira ya saa 12:00 jioni katika Maeneo
mbalimbali ya mji ambapo katika msako huo Askari wakiongozwa na taarifa za
kitengo cha kufuatilia makosa ya mtandao kwa kutumia namba ya muhanga taarifa
zilionyesha mtuhumiwa yupo maeneo ya kindai ambapo kwa haraka Askari walijipanga
kufanya msako mkali eneo hilo hatimaye mtuhumiwa alitupa begi baada ya kubaini
anafuatiliwa. Kutokana na hali ya giza mtuhumiwa hakuweza kutambuliwa vizuri lakini
ni kijana anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka ishirini(20). Aidha baada ya
kuchunguza ndani ya begi hilo vitu vyote vilipatikana kasoro Tshs 120,000/=
pesa ambayo alikuwa ameichukua tayari.
Aidha kuhusiana na tukio hilo hakuna Mtu/watu
wanaoshikiliwa, na Jeshi la Polisi linaendelea na msako kumtafuta Mtuhumiwa ili
akamatwe na kufikishwa Mahakamani ameeleza Mbughi.
Kisha Kaimu Kamanda akatoa wito kwa wananchi wote
kwa ujumla na mashabiki wa mpira kuachana na vitendo vya kihalifu vya
aina yoyote hususani michezoni na kutoa onyo kwa yeyote atakaye thubutu kufanya
hivyo Jeshi la Polisi halitasita
kumchukulia hatua kali za kisheria.
Kocha wa timu ya Singida Uniteda aliyekaa kulia akionesha mkoba wake uliopatikana muda mfupi tu baada ya kuibiwa . Kupatikana na kwa mkoba huo kulitokana na Msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema katika Mji wa Singida. ( Picha kutoka mtandaoni)
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454/0652683063
Namba yetu ya WhatsApp 0629 655814
Facebook - machibya richard.
No comments