ANUSURIKA KIFO, ASHIKILIWA NA POLISI BAADA YA KULAWITI MTOTO HADI KUFA MACHUNGANI
ANUSURIKA KIFO, ASHIKILIWA NA POLISI BAADA YA KULAWITI MTOTO HADI KUFA MACHUNGANI
Jeshi la Polisi
Mkoani Singida linamshikilia Mtu mmoja aitwaye Nalogwa
John (23), Mnyiramba, mkazi
wa Kijiji cha Mgundu, Wilayani
Iramba baada ya kumlawiti mtoto mwenye
umri wa miaka 12 jina lake linahifadhiwa na kumsababishia maumivu makali na
kupelekea kifo kwa mtoto huyo.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kweke jana,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Sweetbert M. Njewike
ameeleza kuwa tukio hilo lilitoke siku ya tarehe 25.08.2018 majira ya saa 11:30. jioni huko
katika kijiji cha Mgundu wakati marehemu akiwa machungani.
Katika picha ni ACP Sweetbert M. Njewike
Kamanda wa polisi Mkoa Wasingida.
ACP Njewike ameeleza kuwa kabla ya tukio hilo
machungani akiwa katika harakati za
kukata fimbo ya kuchungia kichakani na
akiwa na mdogo wake aitwae Abdul
John (9), marehemu alikamatwa kwa nguvu na mtuhumiwa Nalogwa John, kumkaba
shingoni kisha kumlawiti mbele ya mdogo
wake ambaye alikimbia hadi nyumbani na kutoa taarifa kwa Mama yao ambaye alifika eneo la tukio na kukuta mtoto wake
tayari amefariki. Mama huyo alipiga
kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walifika eneo la tukio.
Aidha Kamanda ameeleza kuwa baada ya mtuhumiwa kutenda
kosa hilo alijaribu kutoroka na
kukikimbilia nyumba jirani lakini wananchi walifanikiwa kumkamata na
kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kwa
kutumia fimbo na mawe ambapo Askari wa Jeshi la Polisi walipopata taarifa
walifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuokoa maisha yake.
Njewike ameweka wazi kuwa Mtuhumiwa huyo anashikiliwa
kwa mahojiano zaidi kabla ya kufikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake
na Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Iramba kwa uchunguzi wa Daktari kabla ya kukabidhiwa kwa
ndugu kwa hatua za mazishi.
Hata hivyo Kamanda amewataka wananchi wote wa Mkoa wa
Singida kuachana na vitendo vya kikatili kama hivyo, waache kujichukulia sheria
mkononi na kuwaasa wazazi kuacha kuwatuma watoto wadogo kwenda kuchunga mifugo
wenyewe na kuwaasa wazazi hao kuwapeleka watoto wao shule ili wapate elimu
kwani elimu ndiyo hadhina ya maisha yao ya baadaye.
Kama una Habari, matangazo, Picha, Maoni au ushauri tuma kwa kupitia anwani zifuatazo;
E- mail. -sylvestermac87@gmail.com
-machibya.richard@yahoo.com
Sim No. 0768367454WhatsApp/0652683063
Facebook - machibya richard.
Kiongozi unafanya vizuri sana, umeiva kihabari
ReplyDelete